Wakuu Msaada: Referees Recommendations Forms

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Wakuu habari ya mapumziko? Kwakuwa mtafutaji hachoki nimeona ni vema nikatuma maombi nafasi zilizotangazwa UDOM. katika kusoma maelekezo namna ya kutuma maommbi kuna fomu moja inaitwa referee recomendation form unatakiwa uidownload kwenye website ya chuo. Nimeidownload ukiisoma fomu hii kwanza imeandikwa CONFIDENTIAL kwa maana ya siri na kuna sehemu mbalimbali refa anapaswa kuijaza mfano "ability to work in team" na mengine mengi. Nisaidieni yafuatayo

1. Ukisha idownload unamtumia/unampa refa anakujazia anakurudishia ndo unaiambatanisha na wasifu na barua unatuma?

2. Kama ndivyo hiyo siri (aliyojaza refa) ni kati ya nani nani?

3. Kama ni kati ya refa na chuo je refa akishajaza anapaswa kuituma mwenyewe?

4. Kama marefa wako sasa wako mikoa tofautitofauti inaruhusiwa kuwatumia kwenye email uwatumie wakujazie wascan wakutumie udownload uambatanishe na wasifu na barua utume.
 
Akishajaza anagonga mhuri anaifunga na juu ya bahasha pale unapofunga anagonga mhuri then anakupa unaambatanisha na zingine Kama ya maombi na vyeti Kama yuko mbali nadhani utawsiliana nae uone Njia utakayotumia kumtumia hiyo fomu na yeye atatumia hiyo hiyo kukurudishia
 
Hiyo ni confidential in the sense that Referee akishajaza inabidi aiweke kwenye bahasha ambayo ni sealed (anaweza piga sahihi pale kwenye kifungio au akapiga muhuri, ili wewe usiweze fungua nakujua nini kimeandikwa ndani). Akishafanya hivyo anakurudishia wewe kwaajili ya kutuma pamoja na application yako OVER...
 
Asante Mkuu ERO,GAKATO. Ndo maana naipenda sana jf. Sasa wakuu mfano mimi nigraduate nilifanya field katika manispaa fulani katika kitengo Cha HR sasa ma HR waliokuwa wananikochi ndo huwa nawatumia kama marefa sasa kwa sasa wawili wamehamishiwa mikoa miwili tofauti na mimi niko mkoa mwingine tena tofauti na tofauti na hao sina marefa wanaoweza kunijazia taarifa hizo nifanye nini wakuu wangu.
 
Kla kukicha waajiri wanaamka na jipya bdo tu kuita wazazi wajue nao km wana background ya kazi ama laa....ai dairly complications hawakawii kuwatum vyeti vya nursery ubatizo na ndoa.too boring
 
huu ni ujinga. ndio maana kufoji hakuiishi,refa yupo kigoma mm nipi dar,nitampelekeaje.
sio kwamba nakatisha watu tamaa bt haina maana yoyote.
watasema na vyeti vya chekechea sasa
 
Sasa mareferee si zaid ya mmoja, ukimpa wa kwanza akaijaza halafu akaifunga kwenye bahasha hao wengine wataijazaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…