Wako wapi tuliowapa dhamana????

Joined
Nov 26, 2015
Posts
9
Reaction score
4
Ni kweli Dunia haihusiki moja kwa moja, na ile dhana ya GLOBALISATION ndipo inapokufa kibudu, Ni kweli umoja wa Afrika upo lakini ukiwa na viongozi wasiojitambua na ndipo ile dhana ya Afrika Unite inakufa kifirauni. Nitakuwa mtu wa Mwisho kuitambua Tanzania kama ni nchi ya Kidemokrasia, Nitakuwa wa Mwisho kukaa mbele za watu na Kuwasifu Viongozi wa kisiasa wa Upinzani ya kuwa eti na wao ni watetea wanyonge. Yuko wapi Maalim Seif, yuko wapi Mbowe, Yuko wapi Lowassa, wako wapi wengine wanaojiona kuwa wao ni wapigania haki??? Zanzibar demokrasia imebakwa hadharani, demokrasia ambayo bado ni bikra mbele ya USO wa Dunia, Wazanzibar waliamua tar 25 Oct, lakini mijitu ya miraba minne imewapokonya, nani awapiganiewakati Manyani waliotumwa mjini si Manyani tena?? Nani awatetee wakati watetezi wao wameshakuwa Wanyonyaji kwao??? Hakika naamini aliye juu hana mpango wa kushuka Chini, mwenye shibe hamtambui mwenye njaa. Viongozi wengi huchaguliwa na watu lakini mwishowe si chaguo LA watu, Nawaambieni enyi Watanzania wenzangu mnaoishi Zanzibar, wakija kuwaamsha usingizini watawapa dawa ya usingizi, Amkeni, Amkeni, Amkeni wenyewe, nani amezifumbanyoyo zenu??? Nani amewasahaulishayaliyopita miaka mitano?? Nani amewalisha unga wa Ndele??? Mnamtegemea nani awe Mtolewa?? Hebu jiulizeni mliowaamini bado mnaongea nao lugha Moja????? Sina cha kuwapa ili muijue kesho yenu, lakini neno ningejua huja mwisho wa safari mkiendelea huamini kuwa Zimwi likujualo halikuli likakumaliza mtakuja kushtuka juzi, ilipita, Jana imeisha na leo hiyoooo inayoyoma.
Augustine John P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…