Kama unapajua anapokaa na una uhakika haishi na mtu, mvizie siku moja kabla hajaenda kazini au usiku kabla hajalala. Vaa koti refu bila chupi ndani wala sidiria. Ukifika kwake, mgongee na akifungua tu mlango, vua koti na ubaki kama ulivyizaliwa kisha umkumbatie na kulia haswa. Lia kike bila aibu ukiwa umemng'ang'ania hata kama atafurukuta usimwachie. Ataelewa umemmisi na sitakueleza yatakayofuata maana wewe ni mtu mzima. Baada ya hapo umweleze namna unavyompenda na kama ulikuwa umejisahau katika maeneo fulanifulani muahidi kubadilika. Mpikie, mfulie nguo, mnunulie zawadi na hata kumsaidia vitu vingine hata kama hajasema. Usibweteke hata kama ana pesa, jishaue na kumpatia pesa, usimchungechunge sana wala kumwonyesha wivu wa kitotokitoto na badala yake onyesha kumjali, usiingilie wala kuhoji sana maswala yake ya kikazi au kibiashara isipokuwa pale atakapokushirikisha, kama anavuta sigara au anakunywa pombe, mnunulie na kumletea bila yeye kuomba mradi iwe brand unayojua anatumia.
Mwombe ngono hata kama utaona aibu na uwe mbunifu sana, mwonyeshe utundu mpaka ule wa akiba. Mwanaume hapendi mwanamke asieweza kujibeba, labda huyo mwanaume awe na tatizo la kupenda kumcontrol mtu ndio atataka uwe na character za mtu asieweza kujitegemea maana ukionyesha kuwa strong, kwake ni jambo linalomtia hofu kuwa hataweza kukumudu ambako kwa tafsiri yake huwa ni kukucontrol na kukufanya kama mtumwa fulani hivi. Msome yeye yuko upande gani na kama ni mtu anaependa ujimudu, buni miradi na kuonyesha kiu na bidii ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato chenu.
Kwa haya machache, sidhani kama atatoka mikononi mwako labda iwe ulilala na rafiki yake au mtu yoyote akajua maana hujasema ulichomkosea.