Nilifuatilia ufunguzi wa kampeni wa chama tawala jana pale jangwani na kwa kweli nilisikitika nilichokuwa nasikiliza. Wote waliozungumza hawakuongea jambo la msingi la kuwashawishi wananchi wawachague, ni mashairi na ngonjera tu. Makamba anazungumzia ati wana wabunge 10 tayari, so what? Dr. Bilali anawashukuru wenzie kumteua, so what? Raisi Kikwete anazungumzia walichofanya, mara TUKTA, mara tumepeleka watu mashuhuri mahakamani etc so what? Je hii niishara ya kuonyesha umbumbumbu tulio nao wananchi wa TZ? Umaskini wa kipato ndio umepelekea sisi wananchi kuwa na umasikini wa kufikiri?
Kampeni ni kuwaelezea wananchi utakayowafanyia na namna utakavyotekeleza, that simpo. Sio kupoteza mda kueleza yaliyopita ambayo hayana nafasi kwenye maisha yajayo. Eleza utakavyokusanya kodi, eleza vipaumbele vyako, eleza utakavyoboresha huduma za afya, eleza utakavyokomesha rushwa, eleza utakavyokuza uchumi wa nchi kwanjia unazojua wewe, eleza elimu utafanya nini n.k. Kumpeleka mtu mahakamani sio achievement, haiwezi kukufanya wewe uchaguliwe kutuongoza. Nawashauri wagombea wengine watueleze watakayofanya na namna watakavyotimiza hayo wanayokusudia kufanya, hatuna muda wa kusikiliza porojo zisizo na mantiki.