CHAWADE
S. L. P 90041 Dar es salaam.
Phone: +255 789113534, +255 688 080 063
Mw/Chai - Matombo na Gombero (house No 28)
chamachawade@yahoo.com-
-
VYAMA VYA SIASA VYATUMIKA KUPOTOSHA WATANZANIA
-
Wakati mchakato wa mabadiliko wa katiba ukifikia hatua ya kwanza ya maoni inayotarajiwa kupigwa Aprili 30 mwaka huu, kuna baadhi ya watu wameendelea kubaki njia panda kuhusu suala hili la mabadiliko ya katiba mpya. -Ikiwamo suala hili ni kutaka kufanyika kimaslahi zaidi kwa baadhi ya vyama vya siasa wakidai hawaridhiki na baadhi ya vipengele vilivyotumika katika kuandaa katiba hii mpya. -Ikiwamo pia kususia baadhi ya vikao vya mchakato huo kwa ujumla, hii inaonyesha ni jinsi gani siasa ya Tanzania inavyotumika katika upotoshaji kwa mfano:-
a)-Kuhusu baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kutokubali kuachia ngazi za uongozi -na kufanya vyama hivyo kuwa ni vya kifamilia au kampuni iwapo atajitokeza mwanachama ndani ya chama chochote cha siasa akahitaji kugombea nafasi yeyote ndani ya chama hicho hapewi nafasi zaidi ya kushambuliwa na maneno ikiwemo kutishiwa kufukuzwa ndani ya chama na kunyang'anywa -kadi ya uanachama hata kama ana uwezo na sifa zinazostahili kupata uongozi utamkuta mtu yuko kwenye chama cha siasa -na yuko ngazi za juu za uongozi lakini hana sifa za kuwa kiongozi kutokana -na sifa alizonazo, isipokuwa atapewa madaraka ili mradi awe ni mmojawapo katika familia inayoendesha chama hicho huu ni upotoshaji hili inabidi tulinyooshee kidole na -kuliangalia kwa macho mawili huu ni upotoshaji. -Kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hawaziheshimu katiba za vyama vyao je wataweza kuiheshimu katiba ya nchi? Ikiwamo kuonesha jeuri ya pesa kwa kuzimwaga katika majimbo yao wakati wa chaguzi huu ni upotoshaji pia.
-
Kuna baadhi ya watu wanaotoka katika taasisi za kidini na kujikita katika siasa wakati huko katika taasisi hizo kuna maovu mbalimbali yaliyofanyika ikiwemo ufisadi na ubadhirifu wa fedha na mali za taasisi hizo, huu ni upotoshaji mkubwa ufike wakati watanzania tuseme inatosha.
-
-
-
KUHUSU SAKATA LA "ESCROW"
Sakata hili lilihusisha watu tofauti baadhi yao wakitoka vyama vya siasa ikiwemo chama tawala lakini cha ajabu na kushangaza sakata hili liliwatuhumu viongozi -wa chama tawala peke yao bila kujali sheria ya nchi inasemaje. Hii inazidi kuondoa matumaini na imani kwa watanzania walio wengi. Inasemekana kuna kiongozi kutoka chama cha upinzani aliyepokea fungu la Escrow akiwa nchini Kenya lakini cha ajabu hakutajwa wala kuwajibishwa katika sakata hili. -Mimi kama mtanzania mwenye uchungu na nchi hii nasema ifike wakati tuzinduke, tutoke gizani tuseme "inatosha" kwasababu imani yetu kwa vyama vya siasa imepotea. Tusihadaiwe na lugha nzuri ambazo zitaliangamiza Taifa na watanzania kwa ujumla bila kujali usawa na haki zetu hii ni kwa maslahi yetu na Taifa kwa ujumla.
-
-
ALUTA CONTINUE
-
Mimi katika ujenzi wa Taifa
Shabiri A. Mpaka
Mw/Kiti Chawade Taifa