CCM inazidi kuchoka, hakuna chama cha upinzani kilicho tayari mpaka sasa kushika madaraka.Hii ni kutokana na aina ya siasa tunazoshuhudia kila leo.
0Kama wapinzani wanadhani kuwa ACT-Wazalendo ni janja ya CCM kupunguza kura za upinzani, kwanini wapinzani hao hao waliwafukuza viongozi wakuu wa ACT-Wazalendo kutoka vyama vyao vya awali?
Au nao ni matawi ya CCM ili kuvurugana wao kwa wao?Kama ni kuhofia nguvu ya ZZK ndani ya ACT-Wazalendo, kwanini hawakufuta kesi mahakamani ili kuja kunusuru kura za upinzani kugawanyika?
Ile dhana kuwa ACT-Wazalendo itapunguza kura, kwanini ni ACT-Wazalendo tu? Kama lengo ni kuitoa CCM madarakani, kwanini kila mtu asipigane kivyake mwisho wa siku tusubiri masanduku ya kura yaamue?
Nionavyo mimi vyama vya upinzani havijiamini.