Vyama vya Siasa vinafanya nini?

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,948
Kwa muda mrefu vyama vya siasa vya upinzani vimekuwa vikilalamikia mambo kadhaa, yanayopokonya haki za vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla katika kutimiza nguzo yao ya kwanza ya demokrasia, yaani uchaguzi huru na wa haki. Mambo makuu na ya msingi yanayolalamikiwa:

1) Kiongozi wa chama kimoja, Chama Cha mapinduzi kuwa na haki ya kuunda Tume ya Uchaguzi itakayosimamia haki za uchaguzi, yaani isimamie haki za yeye aliyeiunda na wale anaoenda kushindana nao

2) Wasimamizi wa zoezi la uchaguzi makada wa CCM kwenda kusimamia na kutangaza kura walizopata wao CCM na zile walizozipata vyama vya upinzani

3) Mlezi wa vyama vya siasa kuteuliwa na kiongozi wa CCM ili akasimamie kwa usawa CCM na vyama vingine

4) Vyombo vya dola, na hasa polisi kupokea amri kutoka kwa viongozi wa CCM kwenda kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanywa kwa usawa kati ya aliyewatuma na wapinzani wake

5) Sheria kuu yaani Katiba iliyoundwa na CCM itumike kulinda haki za watu wote wakiwemo wapinzani wa CCM

Vyama vya upinzani kila mara vimekuwa vikilalamikia mambo haya kuwa hayajengi mazingira sawia kati yao na CCM. Na mara kadhaa, vyama vya upinzani mpaka vimekuwa vikiitisha mikutano au vyombo vya habari kuelezea upungufu huu katika mazingira ya demokrasia nchini mwetu.

Kwangu mimi, kiongozi wa chama cha upinzani kuitisha mikutano kuelezea upungufu huu au kuitisha vyombo vya habari kuelezea mapungufu haya, ni ujinga, kuishiwa mbinu na kupoteza muda wa wananchi. Ni sawa na jamii ambayo imeingiliwa na ujambazi, halafu unaitisha mkutano wa wanaofanyiwa ujambazi kuwaeleza kuwa ujambazi ni mbaya badala ya kueleza mbinu zitakazotumika ili kuzuia ujambazi kutendeka katika jamii yao.

Kila raia wa Tanzania anajua kuwa mfumo wetu wa demokrasia ni wa kihuni, vyama vya upinzani vinajua, CCM inajua, viongozi wa CCM wanajua, viongozi wa vyama vya upinzani wanajua, vyombo vya ulinzi na usalama vinajua, na hata waliouweka huo mfumo ovu wanajua pia. Kupoteza muda kuelezea jambo ambalo kila mtu anajua ni kuishiwa mbinu.

Vyama vya siasa vya upinzani, viongozi na taasisi za uongozi ndani ya vyama vya upinzani vinatakiwa kuja kwa wananchi kueleza ni nini vitafanya kuyaondoa haya yote yaliyo kinyume na misingi ya demokrasia na usawa wa ufanyaji wa shughuli za kisiasa. Wawaambie wananchi, nini vyama vitafanya, nini taasisi za uongozi ndani ya vyama zitafanya, nini viongozi binafsi ndani ya vyama watafanya, wananchi wanatakiwa kushiriki kwa namna gani.

Kila Mtanzania mwenye dhamira na nia njema na Taifa letu hawezi kufurahia uwepo wa uhuni au viini macho katika demokrasia ndani ya Taifa letu.

Viongozi wa vyama vya siasa, wayakumbuke maneno ya Mwalimu pale chuo kikuu cha Dar es Salaam aliposema kuwa binadamu unatakiwa kuichukulia haki kama mali yako ya thamani sana. Mwizi akija akaipora, akakimbia nayo, una mambo mawili ya kufanya, moja ni kuacha aende, nawe uwe umepoteza. Uwezekano wa pili ni kumfukuza. Mwizi wako akifika mbele, akakimbilia ndani ya nyumba, akafunga mlango, ukifika pale mlangoni unatakiwa ufanye uamuzi, moja ni kusema nimeshindwa, ukaishia pale na kuondoka, uwezekano wa pili ni kuvunja mlango, lakini ukivunja mlango, utakapoingia hujui humo ndani amejiandaa na nini na ana kitu gani.

Demokrasia, haki na uhuru hutafutwa, hulindwa, hupiganiwa. Anayekunyima usidhani kuwa hafahamu kuwa anakunyima. Anakunyima akiwa anajua zaidi yako juu ya nini anakunyima. Kumpigia kelele anayekunyima haki yako ukitegemea kwa kuwa unampigia kelele atajua kuwa anakunyima, ni kupoteza wakati.

Vyama vya upinzani ni lazima vije na mikakati ambayo vitawashirikisha wananchi kupiga vita dhuluma, kuetetea haki zao na kupigania haki katika uchaguzi. Kulalamika haitoshi, kususia uchaguzi haitoshi. Vyama vya upinzani, taasisi za kiraia, taasisi zinazosimamia demokrasia na utawala bora, wananchi wanaolipenda Taifa letu, wote wanatakiwa kuunganisha nguvu, kugawana majukumu, ambayo yote kwa pamoja yatasaidia kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye ustawi wa demokrasia. Kung'ang'ania kupigania nafasi za udiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa, ubunge na Urais, wakati unajua kuwa hakuna hata chombo kimoja kiiicho huru kusimamia chaguzi, ni ujinga na kutofahamu unachokitaka. Kama vyama vya upinzani haviwezi kuongozi mapambano dhidi ya dhuluma dhidi ya haki na demokrasia, ni aheri vitangaze kujifuta, ili wananchi na Dunia nzima itambue kuwa watanzania hawana uwezo wa kupigania haki zao, wanaishi kwa kudra na hisani za watawala.

Nguvu zote za vyama vya upinzani zinatakiwa kuelekezwa kwenye kupigania haki na usawa wakati wa uchaguzi, na sheria mama yaani Katiba. Uchaguzi kwa sasa ni kupoteza muda.
 
Haya yote inatakiwa upinzani appointment na rais wamuueleze wanayoona hayafai nadhan yote yatashughulikiwa. ..lakin sio njia uliyoandika hapo mwishon...Rais magufuli msikivu sana tatizo wamzungukao wale nina wasi nao
 
Haya yote inatakiwa upinzani appointment na rais wamuueleze wanayoona hayafai nadhan yote yatashughulikiwa. ..lakin sio njia uliyoandika hapo mwishon...Rais magufuli msikivu sana tatizo wamzungukao wale nina wasi nao
Unamzungumzia Magufuli yupi?
 
kama maisha yamekushinda rudi kjijini kwenu ukalime itapendeza zaidi kuliko kujipendekeza kwenye siasa usioyoijua
 
Haya yote inatakiwa upinzani appointment na rais wamuueleze wanayoona hayafai nadhan yote yatashughulikiwa. ..lakin sio njia uliyoandika hapo mwishon...Rais magufuli msikivu sana tatizo wamzungukao wale nina wasi nao

Sina uhakika na uyasemayo. Lakini nadhani mazungumzo yameshindikana. Yakishindikana mazungumzo, options gani zipo? Kule Bunge la Afrika, wabunge wa Tanzania na Burundi waliomba kuwe na mazungumzo kabla ya uchaguzi. Wenzao wamekataa na kuendelea na uchaguzi. mwisho wabunge wa Tanzania wameamua nini?

Kulivyokuwa na malalamiko mwakajana juu ya ugandamizaji wa demokrasia, CHADEMA walidhamiria kufanya maandamano. Viongozi wa dini wakawasihi wayafute (hata mimi sipendi maandamano kama kuna nafasi ya kuongea), CHADEMA wakakubali. Baada ya hapo kilifuata nini? Tunaambiwa tu kuwa waliomba kuwepo mazungumzo lakini ombi lilikataliwa.

Mimi naamini Rais ataungwa mkono zaidi kwa kuonesha ungwana kuliko kuendekeza ubabe.
 
kama maisha yamekushinda rudi kjijini kwenu ukalime itapendeza zaidi kuliko kujipendekeza kwenye siasa usioyoijua

Out of context. Shame on you.
 
Vyama vya upinzani sio viongozi bali waachama ambao ni mimi, wewe, na yule, nikiwa na maana kwamba kama wanachama wa vyama hivi wataungana kwa dhati na kupaza sauti zao kwa ajili ya kudai hizo haki za msingi kabisa na tena wakifanya hivyo bila ya kuchoka na kukata tamaa haki itapatikana tu. Dunia ya leo haki inapatikana kwa kupitia nguvu ya umma na wala sio nguvu ya watawala.
 

Ndiyo maana ukisoma vizuri, kuna eneo nimesema wazi kuwa vyama vya siasa, taasisi zinazotetea haki za raia, makundi ya kijamii, taasisi za wasomi na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa letu, anatakiwa kushiriki katika jitihada za kuifanya Tanzania kuwa nchi inayodumisha haki na misingi ya demokrasia. Ili kukusanya nguvu yenye kuleta matokeo chanya, kunahitajika mbinu ya kuunganisha nguvu na kujenga umoja, na hilo haliwezi kufanywa na kila mtu. Lakini katika jitihada lazima kuwepo miongozo na viongozi pia wanaoainisha mbinu za kukusanya nguvu ya pamoja na kuanisha wajibu wa kila kundi. Hatutaki jitihada zigzag bali mbinu zilizopangwa, zenye kuleta matokeo chanya bila ya kuathiri utengamano wa Taifa.

Yawezekana nakosa taarifa sahihi lakini kwa ujumla sioni jitihada za kuunganisha nguvu za vyama za vyama vya upinzani. Unapotaka mabadiliko, umoja ni jambo la muhimu kuliko kitu chochote. Ni wakati wa kuzika tofauti ndogo ndogo. Kuna sababu gani ya kuendelea kuitenga ACT au Zito wakati nyote mnapokea madhira yale yale?

Kuna jitihada gani za kutafuta umoja na taasisi zisizo za kisiasa lakini zinapigania katiba mpya au demokrasia na haki za raia? Kuna jitihada gani za kuunganisha nguvu na taasisi zinazosimamia vyombo vya habari ambavyo navyo vinashtakiwa na kufungiwa ovyo? Kuna jitihada gani za kuunganisha nguvu na viongozi wa taasisi za dini wanaofunguliwa kesi kila wakati au kuhojiwa kwa vile tu wametamka maneno yasiyowapendeza watawala?

Kwa sasa nilidhani ni muhimu kuunganisha nguvu kutoka kila kona, kisha kupaza sauti kwa namna ambayo anayekunyima haki anatambua kuwa hawa watu wameamua kuitafuta, kuilinda na kuitetea haki yao ya msingi, hawahitaji niwapatie kama hisani bali wanaidai. Watawala ni lazima waongoze kwa matakwa ya wanaotawaliwa na siyo watawala wawaongoze raia kama wanavyotaka.
 
Huu ni uzi wenye mashiko kwa wenye Akili isiyotegemezi kwa maana ya Akili huru
 
Umeandika point tupu, CCM hawawezi kuitoa kwa kulalamika wachukue hatua zozote hata mimi naunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…