Elimu imezikwa rasmi serikali yako unajua kabisa kuwa tunawaangamiza watanzania ,inapita majukwaani kutangaza elimu bure kumbe ni maigizo tu maana hakuna mtoto wa mbunge wala waziri anayesoma kwenye hayo maigizo zaidi ya baada kwa watanzania baada ya kuona wameshindwa kuboresha elimu sasa mbinu zilizobaki ni hizo ambazo unaziona ,kwamba walimu baada ya kudai maslahi yao serikali ikaona hakuna umuhimu wa kuwaboreshea mishahara Wala posho walimu wamegoma kimya kimya maana hakuna chombo cha kuwasemea hapa anzia wakati wa kikwete anachukua madaraka walipewa ahadi nyingi sana ambazo ulitekelezaji ulikuwa mdogo ,mitihani ya msingi na sekondari ikaendelea kwa shingo upande nafikiri matokeo uliyaona yaani ni mabaya kiasi kwamba hata yule mwenye darasa la mwisho amaalipandishwa ili tu wananchi wasijue kinachoendelea hali ile imeendelea mpaka hivi leo na sasa wakuu wa shule wanalazimishwa lazima shule yako ifaulishe usipofaulisha ukuu wa shule unaondolewa ,sasa wakuu wa shule kuogopa kuondolewa kwenye hicho cheo anatumia mbinu zote za kufaulisha yaani anzia shule,kata,wilaya, na mkoa kwa ujumla wake hadi NECTA ili tu magazeti ya muda huo yapambwe na vichwa vya habari vinavyosema UFAULU WAONGEZEKA.Sasa unajiuliza hivi tunatengeneza taifa lipi?Halafu kwa faida ya Nani?