Utumishi

mfirigisi

Senior Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
115
Reaction score
50
jamani niliomba kazi utumishi tangazo la tarehe 25 sep 2014 ingawa bado mpaka sasa hatujaitwa kwenye usaili , kuna kitu nahisi wanaweza wasiniite kwenye usaili nilisahau kuandika kazi ninayoomba juu ya bahasha.....niliposoma maelezo yao usipoandika kazi unayoomba juu bahasha , barua yako inakuwa invalid. mwenye uzoefu anisaidie
 
Pole mkuu, omba Mungu muwe hamkuomba wengi katika hiyo post kwani huwa wanataka uandike juu ya bahasha ili kuepusha usumbufu wa kuchambua bahasha hii ni kwa ajili ya post gani. Kuna rafiki yangu alisahau kama wewe lakini aliitwa. Cha msingi ujitahidi siku nyingine ususahau.
 
Hata mimi nilisahau na nikaitwa.... Ila niliandika post tu sikuandika institution.....
 

Asante sana mkuu kwa msaada wako angalau umenipunguzia hofu niliyokuwa nayo...tatizo ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuomba kazi
 
Kati ya sehemu rahisi kupata kazi hapa Tanzania ni kwa kupita utumishi, utumishi hawajali una GPA ya ngapi, wewe ni wa wapi, umetoka chuo gani(provided inatambulka na TCU).
Mimi ni mmoja kati ya watu niliopata ajira kupitia utumishi na pia marafiki zangu wengi wamepata kwa kupitia utumishi.
back to your request, ili kuitwa kwenye interview ya utumishi( 1st interview) lazima uwe umetimiza masharti yaliyowekwa kwenye tangazo( application tu ya kazi ni first of first interview) ama pia ni sehemu ya mchujo kwani watu ni wengi wanao apply.
Ndugu ni vigumu sana kuitwa kama hukuzingatai utaratibu wa tangazo, but i hope utapata kazi soon kupita utumishi provided umezingatai msharti ya tangazo, Nimeamu kukuambia kwa undani kwani nakumbuka sikuitwa na TAKUKURU kisa niliandika barua kwa kutype.

Main things ya kuzingatia wakati unapeleka barua posta ya kuombea kazi utumishi;
1. Umeandika barua na mkono
2. Umeambatanisha copy ya vyeti husika tu
3.Umeatach vyeti kwa pamoja
4.Umeandika apl juu ya bahasha.
5. Umetuma kwa anuani sahihi ya utumishi
6,umetuma kwa njia ya anuani ya kawaida i mean do not send via EMS,register,
7. Kumuomba Mungu ifike salama.
Nice application na karibu kazini
 
Hiyo point si lazima barua uandike kwa mkono, huwa naomba UTUMISHI barua zangu zote huwa naprint na nimeshauzuria sahili kwa kila niloomba sema bahati si yangu ila Usaili kama kawa kama dawa.
 
Hiyo point si lazima barua uandike kwa mkono, huwa naomba UTUMISHI barua zangu zote huwa naprint na nimeshauzuria sahili kwa kila niloomba sema bahati si yangu ila Usaili kama kawa kama dawa.

Mkuu umenirejeshea pumzi, niliposoma point za mkuu hapo juu nikajua nilishafeli kwa sababu nilitype barua yangu.
 
but barua ya kazi inatakiwa iwe handwritten

Hivi ni kwa nini unakuwa mgumu kuelewa, umeambiwa kuwa, uandike kwa mkono ama utype yote kheri ili mradi ukidhi vgezo. Mbona unang'ang,ania kusema iandikwe kwa mkono? Mimi mwenyewe nimetype mara zote na nikaitwa usaili hata kesho naenda usaili kwa barua niliyotype.
 
tuma application nyingine
 
tuma application nyingine

sasa mkuu nitatumaje nyingine wakati deadline ilikuwa tarehe 8 october 2014 ,nafikiri asa hiv watakuwa walishaanza na ku-shortlist....pia nafikiri ukituma nyingine ndio naweza kuwachokaza nikaonekana muhuni sasa hiv natamani niwafuate kwenye ofisi zao nikawaeleze
 
.
but barua ya kazi inatakiwa iwe handwritten

Kwa dunia ya sasa si lazima barua iandikwe kwa mkono, sababu ya kuweka option ya kuandika kwa mkono ni kwamba bado serikali inaamini kuna vijana watanzania wapo maeneo ambayo hawana uwezekano wa kupata computer au printer, hivyo vijana hawa kama wamekidhi vigezo vya ajira iliotangazwa wasiachwe kwa kigezo cha kukosa computer au printer.

Ila,kama tangazo limeeleza wazi wazi kwamba uandike barua kwa mkono basi hapo ni lazima kufanya hivyo,kwakuwa muajiri atakuwa anataka kupima uwezo fulani
 

Huwwz itwa ht ukaenda kukesha kwa mganga

kama hujaandika post unayoomba juu ya bahasha ni kwamba haifunguliwi.. Inatupwa
 
Huwwz itwa ht ukaenda kukesha kwa mganga

kama hujaandika post unayoomba juu ya bahasha ni kwamba haifunguliwi.. Inatupwa

Ukisema hivyo unakosea kuifungua lazima wataifungua kwa sababu hawajui imetoka wapi na kwanani siyo barua zinazowafikia ni za-maombi ya kazi
 
jamani tuwe serious na application zetu kama kweli tunashida na kazi.unaambiwa barua iwe hand written we unatuma typed, andika post kwny bahasha we hauandiki hata kama ni mara yako ya kwanza kuApply soma maelezo vizuri.

usiwape sababu ya kutokukuita halafu badae uanze kulalamika wanapendelea, hata kama wanapendelea play your part right.

tuwe makini jamani ajira zenyewe za shida hizi usipofanya wanachotaka unategema nini.

Muwe na siku njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…