Utoaji mimba wakina dada

served

Senior Member
Joined
Nov 6, 2013
Posts
168
Reaction score
58
Habari zenu bandugu?

Poleni na majukumu.

Naanza nasimanzi na huzuni moyoni,kiukweli nnaumizwa saana na hili jambo la utoaji mimba kwa nini lakini?

kwa nini?,hebu tufike mahali wadada tuamke,tujitambue kutoa mimba si suluhu.

Maana unakimbia aibu ya muda mfupi na kukaribisha laana ya maisha yako yote hiyo damu itadaiwa mikononi mwako please be carefully kama unajua bado unaupenda ubinti na starehe unazitaka basi watch out sio kuua kiumbe asiye na hatia.

Neno la MUNGU linasema hivi"NTAWAPATILIZA WANA UOVU WA BABA ZAO HATA KIZAZI CHA NNE CHA HAO WANICHUKIZAO"Tazama laana unayoiacha kwa hao wengine utakaowazaa ,namaanisha utakaopenda wewe waishi.Ni hayo tu nawapenda.
 
Si wote wanaotoa mimba wanaepuka aibu, kuna mambo mengi yamezunguka utoaji wa mimba.
 

Not that, i justify but unadhani laana inakuja tu pale kwenye kutoa mimba? "Kuua"?

YULE anayekulaani katika kutoa mimba NDIYE huyo huyo amesema" usiibe, usiseme/usimshuhudie jirani yako uongo" n.k.
Hakuna tofauti kumuita mwingine muuaji, na wewe bado unazini/unaiba n.k
 
^^
Na wanaume tupunguze kuwapa presha zisizo na shingo wala malapa.
Ukiambiwa tu ana mimba yako unang'aka utadhani umepewa tangazo la fumanizi !!
It takes a real man to be a real father.
^^
 
i like this.
^^
Na wanaume tupunguze kuwapa presha zisizo na shingo wala malapa.
Ukiambiwa tu ana mimba yako unang'aka utadhani umepewa tangazo la fumanizi !!
It takes a real man to be a real father.
^^
 
Ni zote ni dhambi LAKINI ni vyema tukatambua kwamba DAMU ya mtoto anayeuwawa itaendelea kudai kisasi.
 


Kosa moja hali-justify kosa jingine.

Kama ingekuwa hivyo hata mzazi wako asingekukataza kufanya baadhi ya vitu kwasababu tu yeye alishavifanya/anavifanya. Hamna mzazi ambae angekuwa anajishughulisha kumfanya mwanae awe bora kuliko yeye. Hamna mwalimu au hata mwana jamii ambae angemkataza mtoto kufanya hiki au kile.

Nwy. . .
Utoaji wa mimba ni jambo ambalo tunatakiwa tujitahidi kulikwepa na kuwasihi wadada/wamama wengine kufanya hivyo hivyo. Kwanza kabisa sio jambo zuri (its unfair) pili ni jambo ambalo wengi wetu (ukiacha wale wanaobakwa/wanaolazimika kutoa kwa sababu za kiafya) tunaweza kujikinga nalo kwa kutoruhusu kupata mimba wakati utayari wa kuzaa hatunao.

Kuna contraceptives za kila aina, kwanini watu wasitumie? Kwanini wasijifunze kuangalia kalenda? Kama mtu hayuko tayari kuzaa kwasababu yoyote ile atumie dawa/condoms/kalenda kuzuia mimba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…