Utalii wa ndani na upandaji miti

ShalomP

Member
Jun 14, 2019
97
154
Ndugu Watanzania wote na wanaJF hapa jamvini kampeni ya upandaji miti, maua ya aina mbalimbali na kuthamini utalii wa ndani bado inaendelea.

Panda miti kwa wingi, unapokata mti kumbuka kupanda mti.

Mazingira unayoishi iwe ni nyumbani kwako au shambani kwako panda walau hata kuanzia mti mmoja, inaweza kuwa miti ya matunda au miti ya mbao.

Huu ni msimu wa mvua tutumie mvua hizi kupanda miti kabla ya Christmas walau uwe umepanda mti hata mmoja.

Nchi ya Libya asilimia kubwa ni jangwa lakini miti ilipandwa wakaibadili Libya kuwa ya kijani, kumbe hata Dodoma tazamia inawezekana kuwa kijani kama Morogoro na Iringa.

Tupande maua kwa wingi, maua huvutia wadudu wa kupendeza kama vile vipepeo.

Maua hufanya mazingira yawe na mandhari ya kuvutia. Maua pia huweza kutumika kama fursa kibiashara.

Kampeni ya upandaji miti na maua unaweza kuanzia hapo hapo nyumbani kwako au kwenu. Tunza mazingira kwa ajili ya kizazi Cha Sasa na kijacho.

Tutembelee vivutio mbalimbali vya utalii tulivyonazo hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama,

Yawezekana gharama za usafiri, vyakula na hoteli kuwa kubwa ndani za hifadhi hufanya watanzania washindwe kufanya utalii wa ndani.

Ombi langu kwa serikali ipunguze gharama kwa watanzania wazawa hii itapelekea kuongezeka kwa utalii wa ndani Akila Mtanzania ataweza kumudu gharama za kutembelea vivutio mbalimbali hapa nchini.

Watanzania mnaoishi nje ya nchi muwe mabalozi wazuri wa kuhamasisha utalii nchini kwa kutangaza vivutio mbalimbali. Hii itaongeza kasi ya kuongezeka kwa watalii.

Tutapata wageni kutoka mataifa mbalimbali Kama vile Ulaya, America, Asia na Afrika.

#Rafiki twenzetu kutalii.
#Utalii wa ndani umechanua.
KuWa mzalendo ipende nchi yako,
Maendeleo hayana chama.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.

Rusha picha mbalimbali za vivutio mbalimbali na mti ulioupanda now Ili wengine wahamasike kwenye uzi huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungeanza na mfano ingependa zaidi.
Pia kwa aina ya Id yako na ukaja na kampeni kama hii dahlia, usitegemee utaeleweka.
 
Serikali kwa kupitia Wizara na Mamlaka husika wangekua wanatoa miche ya miti BURE.
 
Ungeanza na mfano ingependa zaidi.
Pia kwa aina ya Id yako na ukaja na kampeni kama hii dahlia, usitegemee utaeleweka.
Wako watakaonielewa na ambao hawatanielewa,Kila mtu na mtazamo wake.wapo wenye negative attitude,Mi najaribu kushare tu Idea kwa kupeana Elimu kuhusiana na Umuhimu wa kuthamini mazingira yetu.kila mtu na mtazamo wake unaweza kuwa positive or negative,Siwezi kubadili kile mtu anachokiamini mwengine kutalii kwake ni Jambo la muhimu mwengine ataona Kama anapoteza muda.lakini kwa kupitia mada Kama hizi hata wale wenye mitazamo hasi hujifunza kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…