Idea nzuri Mwea. Nina ushauri kidogo na kwakuwa nimekaa vijijini kwa muda na gharama unazosema kidogo na mashaka nazo ingawa sitaki kukukatisha tamaa. Bulb moja kwa sh. 500 ni bei juu kidogo na wastani wa matumizi ya umeme vijijini ni kama sh. 15,000 kwa bulb, TV, kucharge simu. Angalia hili kwanza, pili monitoring ya matumizi ni ngumu sana na wateja si waaminifu hivyo utakuta unaungaza motor kila week na tracing nani anatumia umeme zaidi ni ngumu. Ninachokushauri, kuingia risk ya kuchukua 3m mfanye biashara inaweza kuwa na return nzuri lakini wakati mmepata wateja challenges zitaanza TRA na pili TANESCO watakuwa mgongoni. Nenda REA - Rural Electrification Agency,
http://www.rea.go.tz utapata ideas nzuri za nishati mbadala na kutoa risk kwako na share holders; wewe ni mdau mzuri unaisaidia serikali kupeleka nishati vijijini au sehemu ambazo TANESCO hawajafika, na kwa sababu hiyo kuna mfuko wa fedha kwa ajili hiyo lakini kama unavyojua mambo ya serikali yetu lakini jaribu kwanza ikishindikana then endelea na plan yako ila uwe tayari na ku deal na madenni ya shareholders na kodi za nchi hii..unazalisha umeme vijijini unapigwa kodi juu..mtu anachukua Kilimanjaro Hotel halipi kodi 5 years...upo hapo