Usisononeke, Hali uliyonayo ni ya Muda tu.

satong

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2016
Posts
260
Reaction score
312
Mtu akitaka kupika maharage lazima ayachambue. Wakati wa kuchambua yale yanayoonekana kwa macho ni mabovu hutupwa na yale yanayoonekana mazima hupikwa na kuliwa.

Lakini cha kushangaza, hayo mengine yaliyoonekana ni mabovu mvua ikinyesha huota na kuchanua mpaka unaweza kusikia mama akimwambia mtoto ngo'a tu hayo majani lakini hayo maharage yaliyochanua na kupendeza yawekee udongo yachanue zaidi.

Vivyo hivyo katika maisha, watu wanaweza wasione thamani yako kulingana na hali na mwonekano wako wa sasa na mazingira yanayokuzunguka. Watu wanaweza wakakubagua, wakakutenga na kukutupa kwa kukuona hufai kwa kuangalia hali uliyonayo kwa sasa.

Brother, sister hutakiwi kubishana nao, kaa kimya baraka zako zikianza kukujia watakuona jinsi unavyochanua na kupendeza kama maharage mabichi yaonekanayo yakupendeza yakiwa shambani.

Hali uliyonayo kwa sasa hivi niya muda tu, na wala haitachukua mda mrefu, hakika utachanua tu ila endelea kutenda yampendezayo Mungu.
 
Hakika
Hatupaswi kukata tamaa kamwe. Na dhambi kubwa ni kukata tamaa!! Tuwe na imani kwamba kila mmoja atapata kwa wakati wake. Hali tulonayo ni ya muda tuu, la mno tusichoke kuomba na Kumshukuru Mungu kila leo kwa uzima tulonao!!
 
Maisha hayataki falsafa mfu kama izo..maisha yanataka mtu katili, jasiri, mbishi na asiekubali kushindwa

Mtaendelea kupeana moyo vijiweni na hakuna kitakachobadilika..pigana!
 
Dah! Nataman nilale nikiamka hili limeshapita eee Mungu nitie nguvu
 
Tupambane habari ya kusubiri maharage yaoze, usikubali kutupwa kama hayo maharage mabovu pambana ili upikwe na uliwe
 
fikira za mwenyekiti wa CCM ndio chanzo cha matatizo yote ya watu 50M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…