Ushauri wako ni muhimu sana!

julius mahinya

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
1,152
Reaction score
384
Kwema?
Wana jamvi wenzangu leo nimekuja kwenu kumuombea rafiki yangu ushauri madhubuti kutoka kwenu juu ya yalio msibu! Naomba tumsaidie kwa kuwa yeye si member humu alivyo nielezea nilimshauri lakini nikamwambia ehm tujaribu kupata mawazo ya wenzetu alafu uchanganye na yako tuone kile kilicho sahihi katika hili!

Yeye ana mpenzi wake kifupi wamefikia kuafikiana kama Mungu atapenda basi wataoana, wana muda wa mwaka mmoja katika mahusiano yao! wiki mbili zilizopita alimshitukia mwenzie kama ana mtu mwingine kwani alikua akimpigia simu anakuta yuko busy na mawasiliano muda mrefu sana nyakati za usiku!

Alitaka kujua anaongea na nani muda wote huo binti alimwambia kabla yake alikuwa na jamaa na kwakuwa hakumuuliza kama alikuwa na mtu mwanzoni hivyo naye hakuona haja ya kufanya hivyo! jamaa alimtaka msichana kuamua kama anabaki nayeye au anabaki na huyo jamaa ambaye yuko mkoani Dodoma ila binti na rafiki yangu wao wako Dar wakiendesha shughuli zao za kila siku!

Binti alisema anampenda rafiki yangu na ndio maana aliamua kumkubali huku akiwa na uhusiano wa mwanzo! jamaa akaweka utaratibu wa kumtaka huyo jamaa wa Dodoma asipigiwe simu jamaa naye wa Dodoma alipoona hapigiwi simu hadi yeye apige kifupi baada ya mabadiliko hayo alitaka kujua kulikoni na binti kaamua kumweleza ukweli kisha kumpiga kibuti! Sasa jamaa katishia kuja Dar kudeal nao kadai atakufa na huyu rafiki yangu akifika atafikia kwa binti kwa maelezo yake na hatamtarifu ni lini hilo tamko katoa jana! sasa rafiki yangu hapa hajui nini anafanya!

Ushauri wenu tafadhari!
 
Hakuna haja ya kumuogopa huyo wa dodoma ye kapigwa kibuti af anataka kuwa king"ang"anizi,rafk yako nae yan anaogopa vitisho vya kitoto,nae awe mwanaume si kuogopa ogopa maneno ya mkosaji.
Mbali na hlo huyo mdada anaweza akawa na feelings kwa huyo wa dodoma..
 
^^
Bishanga maajab ya mwanamke kuwa na wanaume wawili au zaidi Hayapo Chit chat tu hata MMU yamejazana ni kiama
^^
 
Last edited by a moderator:
vizuri naona kweli hii point hasa hilo la mkosaji!
 
^^
Bishanga maajab ya mwanamke kuwa na wanaume wawili au zaidi Hayapo Chit chat tu hata MMU yamejazana ni kiama
^^
hili janga la dunia hatuna jinsi kila kitu na wakati wake labda kipindi hiki kikipita kitakuja bora zaidi!
 
hili janga la dunia hatuna jinsi kila kitu na wakati wake labda kipindi hiki kikipita kitakuja bora zaidi!


^^
Ila kweli kwa kizazi cha sasa,,hakuna binti anakubali kuwa na mwanaume mmoja. Mwanamke mpaka anaingia chumbani baada ya harusi haamini kama kweli aliepo mbele yake ni mume wake kweli,,Kama ana nia ya dhati kumuoa avumilie ni changamoto za kila mahali.
Pili wazungumze pamoja wamalize tofauti zao
Tatu.. Awe makini kwani inawezekana ni kundi la mwanamke ambaye anapenda kumfurahisha kila mwanaume
^^
 
Mmmhhhh huyo demu ana matatizo lakin anatengeneza sumu mbaya.....!!!kulikuwa kuna haja gani yakumuacha jamaa wa Dom kwa matashtiti???au ndo anataka kuandikwa historia yakugombaniwa?huyo rafik yako ambwage tu huyo maana hata yeye anaweza asifike safar yake!!!!
 
wote wapumbavuq
Ss ndo nn?
..hapo mwenye maamuzi ya mwisho ni demu,hakuna kingine hapo!
..halafu hyo rfk ako nae c akae pembeni kwanza ausome mchezo!!?nn kujipa tabu?
..na hyo mwanaume wa dom naye mshamba tu,nn kung'angania? Au dem anam entetain?
 

Ha haa haaa, ambwage tu
 
Huyo mwanamke amwambie jamaa wa dom kuwa jamaa anayeishi nae ni usalama wa t..a..i..f..a harafu uone kama atakuja!!
 

Kumbeq usiniambie!?
Basi sawa
 
Kwa ufahamu wangu mkubwa wa hii kitu mapenzi. Jamaa wa Dom wala hana shida ya kurudiana na huyo msichana ila anaugulia maumivu tu. Yeye wazo lake kubwa ni kuharibu tu.
Huyo wa Dom amebwagwa kwa sababu jamaa wa Dar kamuakikishia msichana anamuoa. Kwa msichana yeyote ukitaka fitna muhakikishie unamuoa. Anacho fanya ni kukata matawi wasimzibie rizki. Sasa hapa ndipo moto uwaka, anayechwa ataki kukubali matokeo kirahisi.
Mwambie jamaa yako atulie tu, na awe makini katika maamuzi yake. Wasichana tulio nao ki siku hizi ni wa kushare kawaida. Ampende kupita maelezo, wakiongea jambo walimalize sio kurudia rudia mambo yaliyo pita. Alafu rafiki yako anamapungufu makubwa, kama anaweza kukuadisia mambo hayo basi nyumba yao aitakuwa salama. Ikifikia stage mwanaume unatakiwa uyakabili mambo own by own. Inamaana hata matatizo ya ndoa yao atakuwa anayatoa njee.
 
Wakati mwingine '' we must thing big'', huenda huyo jamaa wa Dom ni sanamu la Michelin limetengenezwa ili kumpa 'pressure' jamaa yako ili afanye mambo kwa haraka. Kuolewa huku, kuna siri nyingi, dada na mama zetu wanajua. Wakati mwingine inabidi sanaa itumike.
 
Kama Mpo Dar ya nini kuogopa?
Dar kuna watu mahiri kama kina
1. Kamuhanda
2 .Mwigulu Nchemba
3. Ramadhan.

Mripoti haraka arudi Dodoma bila Macho na atapigwa bomu.
 
Yeah hali ni ngumu mno! kumjua mtu haiwezekani jamani duh! kuna siri kubwa sana Mungu katuachia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…