Inategemea zinauzwa nchi gani? Vitu vingi ulaya bei zake huwa juu sana ukilinganisha na bongo hata kama ubora ni sawa na sababu wanayotoa ni kwamba wanalipia kodi kubwa sana. Hata hivyo vingine vinaweza kuwa vinafanana lakini vinatoka nchi tofauti, mfano vinavyotoka china ni tofauti na vya ulaya, lakini pia vitu vingi vinavyokuja Afrika nadhani vinapewa punguzo fulani. Ukienda pale mlimani city utaona bei zao ni zinafanana na hizo za mtandaoni wao wanasema vitu vyao ni genuine na hivyo vinalinganishwa na vy ulaya/mtandaoni. Kwa uhakika kama unapesa na unataka kitu ambacho ni cha uhakika, nunua vya mtandaoni kama ni hapa bongo basi nenda na mzoefu anayeweza kukusaidia kujua kipi ni genuine.