UFISADI WA IPTL: HOSEA na Utouh KUMKABIDHI RIPOTI JK badala ya Pinda na Bunge.
Ikiwa ni siku chache tangu Baraza la usalama la Taifa kukutana na kupitia report ya uchunguzi ya PCCB kuhusu ufisadi wa 200bn kwenye akaunti ya Tegeta escrow benki kuu, Taarifa za uchunguzi zinaeleza kuwa mkurugenzi wa PCCB Dr Edward Hosea atamkabidhi Mhe Rais Jakaya Kikwete ripoti hiyo jtano ijayo kama ilivoelekezwa na Baraza la usalama wa taifa. Awali report hiyo ilikuwa akabidhiwe Mhe Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini Taarifa za ndani zinabainisha kuwa uzito wa ripoti hiyo unastahili Mkuu wa nchi mwenyewe kwani kuna maeneo ambayo waziri mkuu atastahili kuwajibika. Mbali na ofisi zilizohusika kwenye ufisadi huu kwa mamlaka yao kama wizara ya fedha, benki kuu, Tanesco, Wizara ya nishati na madini, Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, TRA, na baadhi ya vigogo Ikulu, repoti hiyo imekwenda mbali zaidi kuonesha baadhi ya majina ya watu maarufu waliojipatia fedha hizo kwa namna mbalimbali. Kwa mfano, akaunti ya kampuni ya VIP Engineering katika Benki ya Mkombozi iliyopokea hela za escrow imekutwa hela nyingi zimetoka kwenda kwa wabunge,mawaziri majaji, na baadhi ya watu maarufu (hii ni kwa mujibu wa benki statement ya akaunti hiyo yenye kurasa 27 kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 14 Agosti 2014). Baadhi ya majina ndani ya benki statement hiyo yalitumiwa pesa kupitia akaunti hiyo ni pamoja na Waziri Anna Tibaijuka, Waziri wa zamani William Ngeleja, Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na mmoja wa Majaji wa mahakama kuu ya Tanzania Mujulizi. Katika orodha hiyo kuna Wabunge, wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini, wote isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtumishi mwandamizi wa zamani wa Serikali. Viongozi wawili wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wameonekana katika orodha hiyo pia.
Juhudi kubwa zinafanywa hivi sasa kuzuia taarifa ya CAG na PCCB isikabidhiwe Bungeni kwani itakuwa wazi na kuibua mtikisiko mkubwa nchini.
Taarifa nyingine inasema kuwa baadhi ya wanasiasa walilipwa kupitia akaunti ya kampuni ya VIP iliyopo nchini Uholanzi ambayo hivi sasa imefungwa kwa amri ya benki kuu ya Ulaya ( ECB).