Mimi kuna kitu najiuliza sipati jibu. Hivi hawa maafisa mipango miji huwa wanafanya kazi gani? Kila siku wako maofisini na mishahara wanalipwa. Tena huenda minono. Sasa inakuwaje kuwe na bomoabomoa kama wanapanga miji?
Jiji kama dar ina maana hakuna master plan inayoelekeza nini kijengwe wapi? Hizi bomoabomoa zinahusika either na uzembe wa watu flani ambao hawakifanya kazi zao au rushwa au labda mipango yetu ya miji ni ya miezi sita sita.
Inastaajabisha mji unaokua kama Iringa majengo marefu yanasimamishwa katikati ya mji na wakati barabara ni nyembamba sana. Hakuna hata parking. Halafu baadae tunaambiwa hayo majengo yanayoota kama uyoga yavunjwe kupisha upanuzi wa barabara. Kama manyumbu hivi. Inaudhi na inatia gasara sana.
Naunga mkono hoja mkuu. Bomoabomoa ifanyike nchi nzima, once and for all na ofisi ya mipango miji ifikiriwe upya.