Hadi kesho Chadema kitaendelea kutoa matumaini makubwa kwa Watanzania. Kinachohitajika ni watanzania kukiunga mkono ili matumaini yaweze kufikiwa. CCM wala hatuhiji kulizungumzuia, maana sio tu wameishiwa, bali wapo chini ya kiwango cha kuishiwa, hadi wanaomba kura kwa stile ya kuhurumiwa- ona Arusha wanamtembeza aliyemwagiwa tindikali. Hivi kweli Mwingulu mhitimu wa Chuo kikuu amefikia hatua hiyo? Ya kudhalilisha mtu? Mungu amsamehe bure.
Cuf tusiizungumzie huku bara, labda tu iwe chama kikuu huko zenj.. maana kwa sera za kuokoa jahazi hatutafika mahali... sio tumaini la lolote, bali ni maafa, ni kikwazo, ni Chama hatari kulivyo vyote...
NCCR- ilikuwa mahututi, kama vile hakiwepo tena, ila sasa imevamiwa na waliofukuzwa Chadema, kuna hatari ya hawa kuwa na mpango wa kukidhoofisha Chadema, badala ya kuwa na mpango wa kuleta maendeleo ya Mtanzania. Agenda muhimu ikishakosewa, hakuna matumaini tena.
Taja mengine, matumaini ya pekee yanabaki kwa Chadema tu. Muhimu tuiunge mkono ili tuweze kufikia lengo.
Mungu ibariki Chadema. Mungu ibariki Tanzania.