Usain Bolt asaka viatu vyake

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Viatu vya Bolt vinagharimu pauni elfu 20 hizo ni dola elfu 34 za kimarekani

Mwanariadha huyo bingwa wa Olympic wa mbio fupi sasa ameeingia kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa twitter ulio na zaidi ya mashabiki millioni 3 wanaomfuatilia, akisihi 'jamani najua si tumarafiiki.., aliyeonea viatu vyangu au aliyenavyo tafadhali uvirudishe'!

Viatu hivyo vya michezo rangi ya chungwa chapa cha Puma ,alivyowiweka saini yake vinagharimu pauni za Uingereza elfu ishirini.

Majajusi wa Scotland Yard wanasema viliibwa wiki iliyopia mtaa wa Craydon huko London maeneo ya viwandani vilipokuwa vimeekwa kama maonyesho.

Pia nao wanasihi atakaekuwa na fununu yoyote kuvihusu apige ripoti polisi.

Picha za viatu hivyo alivyovaa Usain alipotwaa ushindi zimezagaa mitandaoni, na sasa anaweka saini pair nyengine atakayoipelekea huko Uingereza.

Wadadisi wanasema itabidi ulinzi wa viatu hivyo uimarishwe zaidi.
Chanzo:BBC
 
wanaotangaza hivyo viatu wanafaulu kupiga promo make na brand ya hivyo viatu, kimsingi hayo ni mafanikio makubwa sana kwa kampuni la PUMA.
 
Kwanini hao puma wasimpe vingine.

Kama ni promo si waseme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…