Nadhani kwakuwa mtaji wako ni mdogo jaribu kuendelea kuwekeza kwenye hivyo vipande vya UTT . Kwa kiasi cha pesa ulichonacho ni very risk ku invest kwenye shares. Unahitaji diversified portfolio na mpaka uwe na mtaji mkubwa lakini kwa kutumia vipande wana kuwa tayari wame diversified. Jaribu kufatilia kipindi ambacho hawajaonnyesha kwenye statement.
Mkuu uliwekeza 7000 after 6 years 24000,,zaidi ya mara tatu faida! Imagine ungekua uliwekeza 10M!!..Thats paying bussiness. Fuatilia hizo figure zilizomiss kwenye statement tu.
vipi ukiwalinganisha na benki za kawaida.. wana unafuu wowote?Mkuu hopaje, huu ni mfuko wa pamoja wa uwekezaji. Katika hali ya kawaida ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kuwa na uwezo wa kununua hisa za kutosha kwenye kampuni zitakazomwezesha kupata faida ya kutosha kutokana na kupata gawio. Wanachokifanya UTT ni kukusanya hela hizi kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi na kutengeneza mfuko mmoja mkubwa ambao utakuwa na uwezo wa kuwekeza kwenye makampuni tofauti tofauti. Hawa wawekezaji wadogo wadogo wengi ndo watakaokuwa wanagawiwa faida itakayokuwa inapatikana kutokana na uwekezaji huo wa UTT.
Hawa jamaa wana mifuko tofauti tofauti kama umoja, mfuko wa watoto, mfuko wa kujikimu na mingineyo ambayo kila mmoja una malengo yake kwa hiyo ni uamuzi wako wewe unayetaka kuwekeza kuchagua mfuko unaoutaka katika hiyo kutegemeana na malengo yako. Waweza tembelea hapa kwa maelezo zaidi: Utt home page
kaka mimi mwenyewe ni mteja utt na hakuna gawio la faida ila wa reinvest faida inayopatikana hvyo pesa uliyo wekeza inapanda na uki hitaji toa faida unaomba statement unaangalia pesa iliozidi unaitoa kwa kujaza form na pesa huingizwa kwenye akaunt yako ndani ya siku kumi..hvyo unakosea sana unaposema utt ni wezi.Hawa ni wezi wakubwa. Wakati wanaanza, walikuwa na lugha laini, kiasi cha kushawishi wengi wetu tukajiunga kwa ahadi nzuri kuwa tutakuwa tunapata gawio. Kinyume chake wamekusanya mamilioni ya Watanzania na kuishia mitini, hakuna cha gawio, na hata ukitaka kuuza hisa zako, wao hawaruhusu, kinyume na ahadi zao za awali. HAWA NI WEZI, SAWA NA UMOJA FUND.
vipi ukiwalinganisha na benki za kawaida.. wana unafuu wowote?
Wadau hata mimi ninampango wa kuwekeza huko. ila baada ya miaka kama mitatu hivi nataka nichukue hela yote nje hii inawezekana
Nashukuru... ni kweli waweza tumia vipande vyako kama dhamana kupata huduma za kifedha kama mikopo na kadhalika?Mkuu kwa uelewa wangu kwa hawa jamaa huwa hawana makato mengi ukilinganisha na yale yaliyopo kwenye mabenki. Makato pekee ninayoyafahamu kwa mfano kwenye mfuko wa Umoja ni 1% pale utakapokuwa unauza vipande. Kwa mfano ukinunua kipande leo kwa bei ya shilingi 200 (huu ni mfano) na ukaja kukiuza kipande hicho labda baada ya mwaka 1 ambapo bei itakuwa shilingi 250, hutauza kipande chako kwa shilingi 250 bali itakuwa shilingi 247.5 (asilimia 1 pungufu).
Nashukuru... ni kweli waweza tumia vipande vyako kama dhamana kupata huduma za kifedha kama mikopo na kadhalika?
Mkuu kwa uelewa wangu kwa hawa jamaa huwa hawana makato mengi ukilinganisha na yale yaliyopo kwenye mabenki. Makato pekee ninayoyafahamu kwa mfano kwenye mfuko wa Umoja ni 1% pale utakapokuwa unauza vipande. Kwa mfano ukinunua kipande leo kwa bei ya shilingi 200 (huu ni mfano) na ukaja kukiuza kipande hicho labda baada ya mwaka 1 ambapo bei itakuwa shilingi 250, hutauza kipande chako kwa shilingi 250 bali itakuwa shilingi 247.5 (asilimia 1 pungufu).