Kuwa mlemavu sio excuse ya kutofanya kazi. Labda tuseme ni ulemavu gani ambao mtu anao. Ni kweli kuna walemavu ambao hata wewe ukiwaangalia unashindwa kujua ni kazi gani hapa duniani anaweza kufanya akapata kipato kama wengine.
Ila kwa tamaa ya pesa, watu wengi wameona ulemavu ni ajira. Hata wale wazima wamekua wanajitia kilema ili nao pia waombe mpaka unashindwa kujua nani wa kusaidiwa na nani anaigiza!
Kwa kiasi fulani, hawa watu wanawadhalilisha walemavu na nashangaa serikali imefumba macho kwenye hili. Pale Ubungo, kuna wakina mama ambao sio hata walemavu, wazima wa afya na wana watoto wao mgongoni wanaomba, ukiwauliza wanasema wana shida - kwani kuwa omba omba ndio solution pekee ya kuondokana na shinda?
Serikali yetu ipo wapi?