Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Ni mawazo ambayo yanaonyesha udhaifu mkubwa
Kama tulivyoona wiki iliyopita, siasa zimeendelea kuwa za mazoea katika nchi yetu, lakini zina madhara. Ni yapi hayo, endelea
CCM inaonekana imepanga mikakati ya kuchakachua; kutokubaliana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba iliyokusanya maoni ya wananchi kuhusu kutupatia tiba ya kero zetu.
Watu wanaomcha Mungu husema, mahali penye ukweli, itafika siku uongo utajitenga.
Mungu na shetani hawakai pamoja. Mungu ni ukweli na shetani ni uongo. Katika maandiko matakatifu, Yesu aliwaambia Wayahudi waliopinga ukweli wake, kwamba wanamfuata baba yao wa uongo, yaani shetani.
Pia, alipigilia msumari aliposisitiza sera ya kwamba, tafuteni daima ukweli na ukweli huo utawaweka huru. Hakuna kitu kizuri, kitamu kama ukweli, kwani unakuweka huru kwa maana ukweli unaleta amani, upendo na furaha. Siku zote, mtu mwongo huwa na wasiwasi na hivi kila wakati hutafuta mbinu za kuutetea uongo wake kwa gharama zozote.
Kuuendesha siasa za uongo na zisizo na uwazi ni gharama zinazozalisha chuki, fitina na mwishowe ni maafa kwa nchi
Mkapa na uwazi
Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alijipambanua kwa sera yake ya Uwazi na Ukweli, sijui kama alifanikiwa kuyaweka mambo wazi au vipi, bado sijafanya uchunguzi.
Mkapa anajua nini kilichofanyika na kama alifanikiwa au la, anajua. Sera ya Uwazi na Ukweli iligharimu maisha ya Yesu Kristo, kwani watawala walipingana naye, wakapindisha mambo, wakawatumia watu vibaya kwa manufaa yao.
Hili ndilo linalofanyika baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutoboa siri ya chama chake.
Kwa vipi? Yeye anaongoza chama tawala kinachojigamba kuwa ndicho kilichoanzisha mchakato wa Katiba ambayo ni sheria mama; kiongozi wake anazunguka nchi nzima akiwaambia wananchi kuwa Katiba mpya haina maana.
Anasema Katiba mpya haitakuwa mwarobaini wa matatizo yao, huku ni kutaka kuwaambia kuwa chama hicho hakina mpango wa kupatikana kwa katiba hiyo, na kama wanayo, basi isiwe na maana kwa wananchi.
Anataka kutuambia wanachofanya wabunge wao ndani ya Bunge la Katiba kuwa ni usanii. Hawapo makini katika kupatikana kwa Katiba Mpya.
Kwa kweli, kiongozi wa namna hii ni maafa na majanga kwa taifa kwani amesikika akienda mbali katika mkutano yake ya hadhara kisiwani Pemba kwamba hata ikipatikana, itaishia kabatini!
Je, huyu ni kiongozi wa namna gani kwa taifa hili? Kwa mantiki hii, kwa nini wanaendelea kupoteza pesa kubaki bungeni na kuendelea na vikao kama wanajua fika kwamba katiba hii haitakuwa na maana?
Ni nani adanganywe
Je, wana- CCM hao wanajaribu kumzuga (kumdanganya) nani? Tuwapongeze Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao wamekuwa na busara ya kujiondoa mapema kwani wameona kwamba hawawezi kuendelea kutwanga maji kwenye kinu. Hao ni wa kweli na wananchi wanawaunga mkono.
CCM ni kama imejikatia tamaa na sasa imeamua kwa makusudi kuvuruga mchakato huu na kumshambulia Jaji Warioba kana kwamba alikaa nyumbani kwake Oysterbay na familia yake, wakaiandika rasimu hii na kuiwasilisha kwa Rais na Serikali yake.
Huu ni upotoshaji unaoonyesha kwamba chama hiki kimechoka kuwaongoza Watanzania na sasa kinataka kuendelea kuwatawala.
Chama hiki kinataka kukwepa hoja na wajibu wa kusimamia Katiba bora, na hivyo kuwaondoa Watanzania katika matumaini ya kujipatia katiba bora na sasa tusubiri bora katiba ambayo haina maana isipokuwa kuweka kabatini.
Mwamko mpya kwa Watanzania
Watanzania wote, lazima tusimame kidete na kuukata upotoshwaji wa namna hii bila kujali itikadi zao, bali kuweka mbele uzalendo wetu. Mtendaji mkuu wa CCM akisimama hadharani na kutamka maneno hayo, haikubaliki hata kidogo.
Tunajua kwamba hakuna Katiba inayoweza kumaliza matatizo ya wananchi, lakini hata hivi hii siyo sababu ya kutoandika katiba nzuri.
Lakini, ukweli ni kwamba CCM lazima itambue kwamba jinsi wanavyopinga rasimu ya Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi na kusimamiwa na Jaji Warioba mtu ambaye ni msomi, mwenye heshima, mwanasheria, mzalendo pamoja na timu yake ya wasomi, basi hivi ndivyo jinsi CCM inavyoendelea kujikaanga kwa mafuta yake na hatimaye kupingwa na taasisi nyeti kama za dini, na nyinginezo.
Tumesikia taasisi kama Kanisa Katoliki ambalo limetoa ujumbe ambao kwa mwenye akili lazima utafika mahali utambue kwamba kanisa hilo linapendekeza nini kutokana na kauli yake ya kulitahadharisha Bunge la Katiba kuheshimu maoni ya Tume ya Warioba.
Taasisi nyingine, Jumuiya ya Kikristo (CCT), taasisi ya dini ya Kiislamu na Umoja wa Wainjilisti, chini ya uongozi wa Mchungaji Bulegi haukurudi nyuma kuunga mkono rasimu ya Warioba na timu yake, lakini ikaonya juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi kuingizwa kwenye Katiba Mpya, jambo ambalo ni uhimu kuliangalia kwa mapana yake.
CCM ijiulize swali
Kwa uhalisia huu je, CCM hapa imebaki na nani? Kama ni wana-CCM wapo wangapi nchini?
Ukweli ni kwamba kama madhehebu ya dini peke yake yatafanya kampeni ya kuikataa katiba itakayokuwa na mapendekezo ya CCM, basi ni wazi Katiba hii haitaweza kupita na haitafika popote na hapo ndipo itakapoishia kabatini kama alivyojisemea Kinana. Ninaona huu ni utabiri mzuri kwa maana ndiko Katiba hii Mpya inakoelekea .
UKWELI UTAKUWEKA HURU: Kweli Kinana shujaa, jasiri anayetoboa siri ya CCM - Makala - mwananchi.co.tz