UKWELI UTAKUWEKA HURU: Kweli Kinana shujaa, jasiri anayetoboa siri ya CCM

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,025
2,000
Ni mawazo ambayo yanaonyesha udhaifu mkubwa

Kama tulivyoona wiki iliyopita, siasa zimeendelea kuwa za mazoea katika nchi yetu, lakini zina madhara. Ni yapi hayo, endelea…

CCM inaonekana imepanga mikakati ya kuchakachua; kutokubaliana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba iliyokusanya maoni ya wananchi kuhusu kutupatia tiba ya kero zetu.

Watu wanaomcha Mungu husema, ‘mahali penye ukweli, itafika siku uongo utajitenga.’
Mungu na shetani hawakai pamoja. Mungu ni ukweli na shetani ni uongo. Katika maandiko matakatifu, Yesu aliwaambia Wayahudi waliopinga ukweli wake, kwamba wanamfuata baba yao wa uongo, yaani shetani.

Pia, alipigilia msumari aliposisitiza sera ya kwamba, “tafuteni daima ukweli na ukweli huo utawaweka huru”. Hakuna kitu kizuri, kitamu kama ukweli, kwani unakuweka huru kwa maana ukweli unaleta amani, upendo na furaha. Siku zote, mtu mwongo huwa na wasiwasi na hivi kila wakati hutafuta mbinu za kuutetea uongo wake kwa gharama zozote.

Kuuendesha siasa za uongo na zisizo na uwazi ni gharama zinazozalisha chuki, fitina na mwishowe ni maafa kwa nchi

Mkapa na uwazi


Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alijipambanua kwa sera yake ya “Uwazi na Ukweli”, sijui kama alifanikiwa kuyaweka mambo wazi au vipi, bado sijafanya uchunguzi.
Mkapa anajua nini kilichofanyika na kama alifanikiwa au la, anajua. Sera ya Uwazi na Ukweli iligharimu maisha ya Yesu Kristo, kwani watawala walipingana naye, wakapindisha mambo, wakawatumia watu vibaya kwa manufaa yao.

Hili ndilo linalofanyika baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutoboa siri ya chama chake.

Kwa vipi? Yeye anaongoza chama tawala kinachojigamba kuwa ndicho kilichoanzisha mchakato wa Katiba ambayo ni sheria mama; kiongozi wake anazunguka nchi nzima akiwaambia wananchi kuwa Katiba mpya haina maana.

Anasema “Katiba mpya haitakuwa mwarobaini wa matatizo yao”, huku ni kutaka kuwaambia kuwa chama hicho hakina mpango wa kupatikana kwa katiba hiyo, na kama wanayo, basi isiwe na maana kwa wananchi.

Anataka kutuambia wanachofanya wabunge wao ndani ya Bunge la Katiba kuwa ni usanii. Hawapo makini katika kupatikana kwa Katiba Mpya.

Kwa kweli, kiongozi wa namna hii ni maafa na majanga kwa taifa kwani amesikika akienda mbali katika mkutano yake ya hadhara kisiwani Pemba kwamba hata ikipatikana, itaishia kabatini!

Je, huyu ni kiongozi wa namna gani kwa taifa hili? Kwa mantiki hii, kwa nini wanaendelea kupoteza pesa kubaki bungeni na kuendelea na vikao kama wanajua fika kwamba katiba hii haitakuwa na maana?

Ni nani adanganywe


Je, wana- CCM hao wanajaribu kumzuga (kumdanganya) nani? Tuwapongeze Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao wamekuwa na busara ya kujiondoa mapema kwani wameona kwamba hawawezi kuendelea kutwanga maji kwenye kinu. Hao ni wa kweli na wananchi wanawaunga mkono.

CCM ni kama imejikatia tamaa na sasa imeamua kwa makusudi kuvuruga mchakato huu na kumshambulia Jaji Warioba kana kwamba alikaa nyumbani kwake Oysterbay na familia yake, wakaiandika rasimu hii na kuiwasilisha kwa Rais na Serikali yake.

Huu ni upotoshaji unaoonyesha kwamba chama hiki kimechoka kuwaongoza Watanzania na sasa kinataka kuendelea kuwatawala.

Chama hiki kinataka kukwepa hoja na wajibu wa kusimamia Katiba bora, na hivyo kuwaondoa Watanzania katika matumaini ya kujipatia katiba bora na sasa tusubiri ‘bora katiba’ ambayo haina maana isipokuwa kuweka kabatini.

Mwamko mpya kwa Watanzania


Watanzania wote, lazima tusimame kidete na kuukata upotoshwaji wa namna hii bila kujali itikadi zao, bali kuweka mbele uzalendo wetu. Mtendaji mkuu wa CCM akisimama hadharani na kutamka maneno hayo, haikubaliki hata kidogo.

Tunajua kwamba hakuna Katiba inayoweza kumaliza matatizo ya wananchi, lakini hata hivi hii siyo sababu ya kutoandika katiba nzuri.

Lakini, ukweli ni kwamba CCM lazima itambue kwamba jinsi wanavyopinga rasimu ya Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi na kusimamiwa na Jaji Warioba mtu ambaye ni msomi, mwenye heshima, mwanasheria, mzalendo pamoja na timu yake ya wasomi, basi hivi ndivyo jinsi CCM inavyoendelea kujikaanga kwa mafuta yake na hatimaye kupingwa na taasisi nyeti kama za dini, na nyinginezo.

Tumesikia taasisi kama Kanisa Katoliki ambalo limetoa ujumbe ambao kwa mwenye akili lazima utafika mahali utambue kwamba kanisa hilo linapendekeza nini kutokana na kauli yake ya kulitahadharisha Bunge la Katiba kuheshimu maoni ya Tume ya Warioba.

Taasisi nyingine, Jumuiya ya Kikristo (CCT), taasisi ya dini ya Kiislamu na Umoja wa Wainjilisti, chini ya uongozi wa Mchungaji Bulegi haukurudi nyuma kuunga mkono rasimu ya Warioba na timu yake, lakini ikaonya juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi kuingizwa kwenye Katiba Mpya, jambo ambalo ni uhimu kuliangalia kwa mapana yake.

CCM ijiulize swali


Kwa uhalisia huu je, CCM hapa imebaki na nani? Kama ni wana-CCM wapo wangapi nchini?

Ukweli ni kwamba kama madhehebu ya dini peke yake yatafanya kampeni ya kuikataa katiba itakayokuwa na mapendekezo ya CCM, basi ni wazi Katiba hii haitaweza kupita na haitafika popote na hapo ndipo itakapoishia kabatini kama alivyojisemea Kinana. Ninaona huu ni utabiri mzuri kwa maana ndiko Katiba hii Mpya inakoelekea .

UKWELI UTAKUWEKA HURU: Kweli Kinana shujaa, jasiri anayetoboa siri ya CCM - Makala - mwananchi.co.tz
 

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,088
2,000
Ni wazi kuwa suala la katiba mpya limeshashindikana.

It is an absolute FAILURE.

Suala hili limeshindikana baada ya ccm kuamua kuingiza maslahi ya kisiasa, makundi na ubinafsi.
Hali iliyopelekea ubaguzi, udikteta, uchochezi, uzandiki na mipasho ktk BMK.

UKAWA wameandika historia nzuri sana itakayodumu vizazi kwa vizazi !
 

kill

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,830
0
kinana ni mnafiki mkubwa anafanya kazi ya wapinzani analalamika mawaziri mizigo kila siku lakini aliyewateua ameziba masikio ni aibu kubwa kwa viongozi wa ccm kuwadanganya wananchi kwa ahadi hewa ccm ni chama cha wahuni na washenzi wakubwa wanalindana wezi wote
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Salamu za dhati ziwafikie wanaCCM na CCM yao. Wakae wakijua kuwa kinachotokea sasa ni mabadiliko. Ni phase muhimu katika demokrasia kokote ilikowahi kuweko, hasa baada ya watawala kugeuza demokrasia kuwa ni uwanja wenye uhuru wa kugeuka kutoka kuwa viongozi, mpaka kuwa fisi, wenye uroho na uchu wa kula mpaka mifugo.

Kitu kimoja ninachojua ni kuwa hakuna sehemu yoyote ambapo wananchi walitaka (demand) mabadiliko na yakashindikana. Wanachokifanya CCM sasa hivi, kitapelekea kutokea machafuko tu nchini, lakini mwisho wananchi watashinda...they always do.

Ni vema CCM ikajiandaa mentaly. Kama bado wanadhani hii vita ya ni Upinzani vs CCM, wanashindwa kuona mbali. This is definitely not that. This is Wananchi vs Udhalimu. So ni vizuri wakajifunza kutokana na historia ili kuiepushia nchi hii umwagaji damu usio na lazima kabisa.

Wakati ambapo nina uhakika kuwa mabadiliko hayaepukiki, bado sijajua itakuwa ni kwa gharama gani. Itakuwa ni aibu kama itawalazimu wananchi kununua uhuru wao kwa damu yao, kutoka kwa waafrika wenzao na mbaya zaidi Watanzania wenzao, wenye roho za fisi, kwani ni wazi huko ndiko wanakotupeleka!


evolution of ccm.jpg
 

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,650
1,250
ulianza vizuri,ulipofika sehemu ya kumtaja mkapa ndio umeharibu habari yako,unamtaja mkimbizi aliyekimbia kwao mtwara,aliyekimbia ndugu zake,aliyewakana ndugu zake kwamba yeye si raisi wa mtwara,mbona obama hakuwahi kutamka kwamba yeye si raisi wa kenya,baba wa taifa aliwahi kusema mkataa kwao mtumwa.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,258
2,000
Mimi huwa ninawashangaa baadhi ya watu wanaojenga hoja za kitaifa na kuanza kuweka mifano ya kwenye kitabu kimoja cha dini kama vile taifa zima lina dini moja.

Kimantiki, hoja za aina hii ni za kibaguzi kwa sababu siyo wasomaji wote wanaoamimi maandiko ya nukuu ulizoleta.

Kama ni kutoa mifano, huhitaji kutoa kutoka kwenye kitabu kimoja cha dini otherwise, nukuu vitabu vyote vya dini kama ni hoja ya kitaifa.
 

Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,080
1,225
Muda si mrefu CCM watasema Kinana sio raia wa Tanzania na kumfungulia mashtaka ya ujangili na wizi wa nyara za nchi.
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,376
2,000


CCM ijiulize swali


Kwa uhalisia huu je, CCM hapa imebaki na nani? Kama ni wana-CCM wapo wangapi nchini?

Ukweli ni kwamba kama madhehebu ya dini peke yake yatafanya kampeni ya kuikataa katiba itakayokuwa na mapendekezo ya CCM, basi ni wazi Katiba hii haitaweza kupita na haitafika popote na hapo ndipo itakapoishia kabatini kama alivyojisemea Kinana. Ninaona huu ni utabiri mzuri kwa maana ndiko Katiba hii Mpya inakoelekea .

UKWELI UTAKUWEKA HURU: Kweli Kinana shujaa, jasiri anayetoboa siri ya CCM - Makala - mwananchi.co.tz


kaka ndio maana wanawatisha kanisa kuwa UKAWA wanataka kuanzisha Nchi ya KIISLAM.
 

daniel merengo

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
278
0
Kinana ni mtu mmoja hatari sana katika ustawi wa nchi hii. eti anwaambia wananchi kwamba serikali ya ccm imewaibia kwa mda mrefu sana halafu anawapa kibwagizo ccm oyee, mazuzu kwenye mkutano wa hadhara yanaitikia OYEE! hii ni hatari sana. weka mbali ni watoto wa tembo na twiga
 

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,025
2,000
ulianza vizuri,ulipofika sehemu ya kumtaja mkapa ndio umeharibu habari yako,unamtaja mkimbizi aliyekimbia kwao mtwara,aliyekimbia ndugu zake,aliyewakana ndugu zake kwamba yeye si raisi wa mtwara,mbona obama hakuwahi kutamka kwamba yeye si raisi wa kenya,baba wa taifa aliwahi kusema mkataa kwao mtumwa.

Habari hiyo sikuandika mimi nimeitoa kwenye mtandao wa gazeti la Mwananchi,
UKWELI UTAKUWEKA HURU: Kweli Kinana shujaa, jasiri anayetoboa siri ya CCM - Makala - mwananchi.co.tz
 

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Kinana anajua anachofanya na in fact kitakuja kuwagharimu sana Wapinzani kama wasipokuwa makini.Kinana anajaribu kuijenga upya taaswira ya CCM kwa wananchi kwamba CCM ya Kinana ipo thabiti kuiwajibisha serikali pale inaposhindwa ku-deliver.CCM inajaribu kujenga hoja kwamba ndani ya Chama chao utamaduni wa kukosoana na kuwajibishana uko well and alive na kwamba CCM yake ipo tofauti kabisa na serikali.Yaani hapa Dr wa Ndovu anajaribu kujenga hoja kuwa wakati serikali ina msimamo huu na Chama nacho msimamo wake ni huo.Sad thing is,Kuna wananchi wengi watamwamini kwa kumuona Kinana kama mwenzao na hiyo inamaanisha watakuwa wanaiamini CCM all over again.Kinana is in fact killing two birds with one stone here:First,He is remaking CCM brand; Second, He is retooling CCM message to the Tanzanians.He is a good political strategist indeed.
 

Bobwe1

JF-Expert Member
Apr 8, 2014
396
0
Mimi huwa ninawashangaa baadhi ya watu wanaojenga hoja za kitaifa na kuanza kuweka mifano ya kwenye kitabu kimoja cha dini kama vile taifa zima lina dini moja.

Kimantiki, hoja za aina hii ni za kibaguzi kwa sababu siyo wasomaji wote wanaoamimi maandiko ya nukuu ulizoleta.

Kama ni kutoa mifano, huhitaji kutoa kutoka kwenye kitabu kimoja cha dini otherwise, nukuu vitabu vyote vya dini kama ni hoja ya kitaifa.

Kama umeafiki hoja sema ndiooooooooo kama hujaafiki sema siooooooooooo.....network failure.....!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom