UKAWA, nani yuko tayari kupoteza?

Nyakarungu

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Posts
472
Reaction score
377
UKAWA NANI YUKO TAYARI KATI YENU KUPOTEZA?

Angalizo,...


Naomba upitie post yangu ya May 11 at 4:05pm, niliyoongea kuhusu mafanikio kutokana na mtu au kundi moja kujikanakinafsi/ kukubali kupoteza maslahi binafsi (sucrifice) na kujitoa wakfu (commitment) ili kufikia mafanikio. Kisha usome hii ya leo ndipo utanielewa tutakwenda pamoja.

Habari zenu Watanzania, naandika hili likiwa wazo huru nikiwa mtanzania ninaetamani kuona demokrasia ikishamili.


Je CUF iko tayari kwa dhati kupoteza maslahi binafsi ya chama kwa mafanikio ya UKAWA?

Je Chadema iko tayari kwa dhati kupoteza maslahi binafsi ya chama kwa mafanikio ya UKAWA?


CUF inapoahidi kuachia eneo la zanzibar ili kumruhusu naibu katibu wa chadema visiwani agombee na inapokubali kuacha maeneo yote yanayoshikiriwa na wabunge wa chadema ili chadema ishinde ni dalili ya ukomavu na utayari wa kupoteza maslahi binafsi ya chama kwa mafanikio ya UKAWA.


Kitendawili kipo kwa chadema nao kuwa tayari kukubali kupoteza maslahi binafsi ya chama kwa mafaniko ya UKAWA.


Je chadema itakuwa tayari kuachia nafasi ya ugombea urais kwa mafanikio ya Ukawa?

Je Cuf iko tayari kukosa nafasi ya mgombea urais kwa maslahi ya UKAWA?


NAFASI ZA UBUNGE SIO KIGEZO SANA CHA KUPIMA UMOJA WA UKAWA KWA SABABU PENGINE CUF IMEJIPIMA NA KUGUNDUA HAINA USHAWISHI KATIKA MAJIMBO HUSIKA KILIYOYAACHA KWA AJILI YA CHADEMA,


Mtihani unakuja kwenye kipengere cha kukubali kukosa mgombea Urais atakaekinadi chama na pengine kuwezesha chama kupata wabunge na madiwani wengi.

Kila upande unapopima faida ya kuwa mgombea urais na kumkosa, kwa kweli faida ya kuwa na mgombea mmoja wa ukawa ni ndogo kwa chama binafsi ila faida ni kubwa kwa umoja wa UKAWA na Taifa.


JE NANI KATI YAO YUKO TAYARI KUPOTEZA KWA AJILI YA TAIFA NA UMOJA BILA VISINGIZIO?


Tusije tukasubiri mwisho tukapewa sababu za uongo zilizojaa unafiki na ubinafsi.


UTASHI NI MTU.



 
Ni kweli kabisa mkuu...changamoto kubwa iko kwenye urais...na hali ya kiuchumi ya chama kimoja kimoja baada ya uchaguzi
 
 
Achana na UKAWA wewe, kahangaikie maigizo yenu ya ACT
 
Una tatizo gani?. Sijawahi kuona umeandika pointless kama leo. Mengine unapaswa kuishia kuwaza siyo lazima upost hapa.

Nadhini kuna kitu hakiko sawa kichwani mwako. Pole sana!
 
kama unasema CUF wamejipima na kuweza kuwaachia chadema pale walipoona hawana uwezo wa kushinda ubunge watashindwaje kujua kwamba katika uchaguzi uliopita ni nani alifuatia kwa kura nyingi baada ya Kikwete?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…