kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,121
- 24,399
Uingereza yakataa kushirikiana na Marekani katika mashambulizi dhidi ya Syria
Gazeti moja la Uingereza limefichua kwamba, Waziri Mkuu wa nchi hiyo amekataa ombi la Rais wa Marekani la kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Syria.
Gazeti la Times limeandika katika toleo lake la leo kwamba, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, amesema katika mazungumzo yake ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani kwamba London inahitaji nyaraka na ushahidi zaidi ili kuweza kushiriki katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria.
Gazeti la Times limeongeza kuwa, Donald Trump hakuweza kumshawishi Theresa May katika suala la kushiriki Uingereza katika vita na mashambulizi dhidi ya Syria.
Gazeti hilo la Uingereza limeandika kuwa, Jumatatu iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alisema kuwa, katika kipindi cha masaa 48 yajayo Washington itachukua uamuzi juu ya suala la kuishambuilia Syria kutokana na madai ya utumiaji wa silaha za kemikali lakini inaonekana kuwa, kadiri masaa hayo yanavyoyoyoma ndivyo kiongozi huyo anavyolegeza kamba na kurudi nyuma.
Marekani na nchi kadhaa za Magharibi zinaituhumu serikali ya Rais Bashar Assad wa Syria kuwa imetumia silaha za kemikali dhidi ya watu wa eneo la Duma huko Ghouta Mashariki, madai ambayo yanapingwa vikali na Syria na Russia.