Uchakavu wa injini na hasa engine valve seals na piston rings husababisha mafuta kuvuja kwa ndani na kuingia ndani ya injini na kuchanganyika na petrol au dissel, matokeo yake ni kuunguzwa na kutoa moshi usio wa kawaida. Kwa sababu hii ukiweka oil leo, baada ya kufanya safari yoyote utakuta oil imepungua.