sawa..!Sijapiga ramli, sina upande nilio egemea maana kila kitu kipo wazi. Atakeyebeba ubingwa atakua amestahili kwa juhudi
Uliyo yaeleza yote nakubalaiana na wewe ila trust me Yanga haitochukua Ubingwa!! Ngoja uone round ya pili ya VPL baada ya mapumziko watakavyo anza kupoteana. Na hapo ndio migogoro baina ya uongozi na wachezaji inapoibuka na kuleta mgomo baridi kwa wachezaji. Pia kama Simba Sc watatolewa kwenye mashindano ya CAF watakuja kwa kasi sana ya kuhakikisha mwakani wanashiriki tena mashindano hayo
Kuwabeba SimbaNa marefa waendelee hivi hivi
Hili ndilo linaloigharimu Simba SC kwa sasa. Morali ya upambanaji iko chini sana sijui kwa nini ila mi nadhani wachezaji wake wameridhika sana ukilinganisha na mahitaji sa timu kwa sasaKikosi cha Simba SC Tanzania ukikitizama katika mechi zake nyingi fighting spirit yake ipo chini au unaweza kusema ni ya kawaida sana, wanacheza mpira mwingi katikati ila huko mbele kumepoa
umesema kweli comrade simba kuna wachezaji wa viwango vya juu ila shida ni jinsi wanavyocheza utashagaa sasa sijui huwa ni maagizo ya kocha ama ni nini kwakweli njinsi yanga wanavyopambana uwanjani mwanzo mwisho ubingwa mwaka huu simba hakuna matumainiSIMBA &YANGA 20/21 MBIO ZA UBINGWA
1. UBORA WA VIKOSI
Simba SC Tanzania ina kikosi bora zaidi ya Young Africans Sports Club
2. MAKOCHA
Makocha wa timu zote mbili hawana CV kubwa sana. Sven wa Simba mafanikio yake makubwa ni kubeba kombe la mataifa ya Africa (AFCON) akiwa kama kocha msaidizi
Cedric Kaze huyu amewahi kupita academy ya Barcelona kama kocha, akaenda zake CANADA.
Kinachokuja kuwatofautisha ni aina ya futiboli wanayofundisha na mifumo. Sven wa Simba anaamini sana katika 4-2-3-1 mfumo ambao anaanza na mshambuliaji 1, kitu ambacho mashabiki wamekua wakilalama aanze na washambuliaji wawili.
Wakati Kaze akiamini sana katika 4-3-3 ambao unampa matokeo sana kwa sababu namba 3 hapa chini.
3. FIGHTING SPIRIT (MORALI YA UPAMBANAJI)
Kikosi cha Simba SC Tanzania ukikitizama katika mechi zake nyingi fighting spirit yake ipo chini au unaweza kusema ni ya kawaida sana, wanacheza mpira mwingi katikati ila huko mbele kumepoa
Yanga kitu pekee kinachowabeba ni FIGHTING SPIRIT, na hichi ndiyo kinaweza kuipa UBINGWA WA VPL 2020/2021. Wachezaji wa Yanga wanajituma sana, wanaonesha hamu ya kulitaka goli hata kama wameshatangulia kupata goli tofauti na Simba Sc wakipata goli 1 wanaanza kupoa na shida ya Simba wakitanguliwa ndiyo inakua mtihani sana.
Yanga wao wakitanguliwa, wanapambana sana kuchomoa goli na kutafuta bao la ushindi.
UBINGWA WA LIGI KUU 2020/2021
Kama Yanga wanautaka Ubingwa, waendelee kuwa na fighting spirit hii hii waliyonayo.
Kama Simba wanataka kuchukua kwa mara ya 4 mfululizo taji hili, wacheze kwa kupambania timu zaidi waoneshe ari zaidi.
Mashibiki mbona haturidhiki?? Huyu kocha kosa lake ni lipi? Tatizo siku hizi kila mtu anajifanya mchambuzi wa soka..Simba ya msimu huu sidhan maana hawaelewek kabisa, kocha anapanga panga tu .
Kitu kingine Simba wanapenda sana mpira wa kucheza na jukwaa na umeongea ukwel Simba wakifunga goli moja wanaridhika na wakitanguliwa mara nyingi kurudisha inakuwa ngumu kabisa ,wachezaj wengi wapo soft Sana kulinganisha na wale wa yanga.
Mimi ni Simba dam ila kwa mwendo huu Sina uhakika Sana na ubingwa kwa msimu huu ,labda wamtoe kocha maana ana kibur Sana yule jamaa pia anaonekana hatak ushaur kabisa