Uwekezaji wetu wa kitanzania ni sifuri kabisa, karibia vituo vyote system yao ni moja.....nadhani kuna msukumo hafifu sana wa kuvutia kazi zenye viwango,weledi, ubunifu....sio kwenye vipindi vya kawaida, matangazo ya biashara, tamthilya, vichekesho n.k.
Huwa naangalia wenzetu wa citizen tv ya Kenya...vipindi vyao, matangazo ya biashara, tamthilya zao na komedi zao ni za kutumia akili na weledi, sio kama kwetu za kuunga unga tu....na kuigana igana toka tv moja kwenda nyingine.
EATV walau wanajitahidi ukilinganisha na wenzao, marekebisho kadhaa, mfano komedi za kina Bambo wawekeze kwenye akili waache kuendekeza yale madudu ambayo nadhani hata mzee Mengi huwa haangalii lakini sisi anaona inatufaa....wajifunze kwa "papa shirandula" ya citizen.