Tutafakari pamoja

maiyanga1

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,409
Reaction score
1,968
Tupo kwenye maombolezo kwa muda wa siku 21 kutokana na kifo cha mpendwa wetu Hayati J.PM.

Mengi yanasemwa kuhusu kifo chake, hata mwenyewe alisema kifo ni kifo, kiwe cha kansa, changamoto ya kupumua, malaria, ajali na sababu nyingine iwayo yoyote. Kila binadamu mwisho wake ni kifo.

Tangu baada ya uhuru kila Rais aliyekuwepo madarakani kwa kipindi chake kuna mambo mengi ya maendeleo yalifanyika.

1. Rais wa kwanza:
Pamoja na kurithi majengo yaliyojengwa na wakoloni yakiwemo mahospitali, maofisi, mashule na miundombinu mingine, na yeye na serikali yake walijenga mashule, mahospitali, vituo vya afya, barabara, madaraja, viwanja vya ndege, reli ya TAZARA, kununua vivuko, kujenga mgodi wa kuzalisha umeme kidatu, kuboresha usafiri jijini Dar kwa kuleta mabus ya Ikarus na miundo mbinu mingine. Lakini bado serikali iliweza kulipa stahiki mbalimbali za watumishi na mshikamano ukawepo. Na kwa kipindi hiki ndio Tanzania ikaingia vitani.

2. Rais wa pili:
Naye na serikali yake aliweza kuendeleza nchi na kujenga miundo mbinu mbalimbali ikiwemo uwanja wa ndege wa pili wa Dar (Terminal Two) mgodi wa umeme Hale, upanuzi wa barabara mbalimbali jijini Dar, kipindi hiki ndio pia vyombo mbalimbali vya habari vilianzishwa kama vituo vya redio na luninga pamoja na magazeti. Pia ndio kipindi ambacho mfumo wa vyama vingi ulianzishwa.
Pamoja na yote hayo bado serikali iliweza kulipa stahiki mbalimbali za watumishi kwa kiwango chake na mshikamano ukawepo.

3: Rais wa tatu:
Naye na serikali yake walijenga mashule, mahospitali, maofisi, barabara, madaraja likiwemo daraja la mkapa, uwanja wa kisasa wa mpira, mgodi wa kuzalisha umeme Kihansi na miundo mbinu mingine pamoja na kuanzishwa kwa vyuo vikuu.
Halikadhalika watumishi waliweza kulipwa stahiki mbalimbali pamoja na changamoto mbalimbali.

Rais wa nne:
Naye na serikali yake aliiendeleza nchi kwa kuendelea kujenga chuo kikuu cha Dodoma, barabara, madaraja, na miundombinu mingine.
Halikadhalika watumishi waliweza kulipwa stahiki mbalimbali na mshikamano ukawepo.

Rais wa tano:
Naye na serikali yake aliiendeleza nchi kwa kuendelea kujenga miundombinu mingine ambayo mingine imekamilika na mingine iko katika hatua mbalimbali ikiwemo ununuzi wa ndege.

Sasa tuna Rais mpya wa sita ambaye pamoja na mambo mengine ametusihi watanzania tuwe wamoja na tushikamane.
Swali kwa watanzania wenzangu ni lini hatukuwa wamoja na tuliacha kushikamana?
Nini kifanyike ili tuwe wamoja tena na tushikamane?
 
Mfano: kitendo cha baadhi ya watu kufurahia jambo fulani na wakati huo huo kuna watu wanalia na kuomboleza jambo hilo hilo, hii ina maana hatupo pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…