Tuseme tu ukweli jamani kwani, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuseme tu ukweli jamani kwani,

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by JATELO1, Dec 27, 2015.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #23
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  WANAJF;
  Kwanza naomba nideclare kwamba mimi ni Mkristo tena anayejitahidi kwa nafasi yangu kuelewa vema kile ninachoamini. Nikiwa kama Mkristo, msingi wangu wa IMANI umejengwa katika MAANDIKO MATAKATIFU, yaani BIBLIA TAKATIFU. Hivyo, vyote ninavyofanya na maisha ninayoishi yanapaswa yaakisi kile nilichoelekezwa kwenye Biblia. Sasa ndugu zangu, hii Sikukuu ya Kristmas nimekuwa nikisherehekea toka nikiwa mdogo mpaka ukubwani lakni jambo moja ambalo liko wazi ni kwamba HAKUNA UKWELI WOWOTE KATIKA BIBLIA TAKATIFU KWAMBA YESU ALIZALIWA DESEMBA 25. Na kwasababu hii kitu inakosa support ya maandiko matakatifu, hivyo naamini wengi wetu tunaisheherekea tu kwasababu ya MKUMBO na MAZOEA TU. Kama kuna mtu yeyote, Mwanafunzi wa Biblia anayeweza kunisaidia na fungu lolote kwenye Biblia (toka Kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo) basi naomba anisaidie.

  Zaidi ya kukosa suport ya Maandiko Matakatifu, lkn pia hata kipindi chote (Miaka 33) alichoishi Bwana Wetu YESU KRISTO hapa Duniani na hata kipindi cha Mitume, hatuoni kama kuna kipindi Bwana wetu Yesu au Mitume walishhiriki Birth-day ya BWANA WETU YESU KRISTO. Sasa hapo ndipo suali linakuja, je waanzilishi wa hii siku ya Kristmas walikuwa na kusudio gani? na ni kwa nini hii siku imekuwa na mwamko mkuu kiasi hiki katika IMANI YA KIKRISTO wakati hata kwenye BIBLIA TAKATIFU haijaonyeshwa kwamba tunapaswa kuisheherekea.

  Nafahamu kwamba wapo wale watakaonibeza lkn hata Biblia inatuambia kwamba siku ile ATAKAPORUDI BWANA WETU YESU KRISTO KUWACHUKUA WATEULE WAKE kwenda nao MBINGUNI, hakutakuwa na sababu Ohooo mimi sikujua wala mimi nilikuwa naambiwa tu Viongozi wangu wa DINI (ambao naamini hata ukiwauliza kuhusu hii Kristmas watakosa Jibu la kukuambia, labda itakuwa ni Propaganda tu zisikokuwa na support ya kwenye Biblia Matakatifu). Na Biblia iko wazi zaidi kwa kusema; Watu wangu wanakufa kwa kukosa maarifa.

  NB: Siamini kama ni makosa kujadili kitu muhimu kama hiki, kwani sioni tatizo la kueleweshana ktk suala ambalo lina mustakabali wa mambo yetu ya kiimani. Ndiyo maana hata katika baadhi ya Makanisa yetu kuna vipindi vya mjadala katika mambo mbalimbali ya kiimani.

  Nawasilisha.
   
Loading...