Unawaza kuwa na sababu nzuri. Haya Kwanini unataka kushuhudia hiyo vita?
well, nimepata kuishi moja ya hizo nchi na kuitembelea mojawapo...
Ni ukweli kuwa Wajapan walitawala China na kuwatesa sana watu wa wakati huo...Wachina wengi waliikimbia nchi yao na maelfu waliuawa. Pamoja na hayo yote hiyo imekuwa ni historia kwa sasa.
Kwa upande mwingine hili suala la kunyanyasa na kuwatesa Wachina limeshafutika katika mawazo na fahamu za Wajapan kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wao walikuwa superior lakini kwa Wachina imebakia kuwa kumbukumbu mbaya kiasi ya kwamba siku ukitaka kukosana na Mchina basi mwambie ya kwamba anafanana na Mjapan.
Sasa ngoja nirudi kwenye sababu yangu.
Baada ya mateso na manyanyaso hayo yote, dhamira ya Wachina na serikali ya Beijing imekuwa ni kuitawala dunia "take over/control the world" katika nyanja zote kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. China is the new emerging nation, na hilo linawafanya watamani kuwa namba moja kwa kila kitu. Kwa mcho ya nje watu wengi huwaona Wachina kama watu wakarimu na wasio na mawaa, lakini mioyo yao imegubikwa na hila.
Kwa upande mwingine nchi ya Japan, hii nitapenda kuiita "the sleeping giant", ni moja kati ya mataifa waungwana sana...wana kila kitu na hawajaanza kuwa nacho leo wala jana. Kama kungekuwa na taifa ambalo lilipaswa kuwa na chuki juu ya vita au uvamizi wa aina yoyote basi hawa bila shaka wangekuwa na kinyongo juu ya Wamarekani kutokana na mkasa na genocide ya Nagasaki na Hiroshima.
Taifa la China linachofanya ni kuitisha Japan kama mpango wa kulipiza kisasi, na ndio maana kuna vurugu zinazoendelea katika miji ya CHANGSHA, QINGDAO, CHENGDU,SHENZHEN,XI'AN n.k kote huko Wachina wanajifanya kufunja, kuchoma na kuharibu kila aina ya property ambayo ni made in Japan.
SASA HAWA WATU INABIDI WAPEWE ADABU KIDOGO ili wajue ya kwamba sio wao tu pekee ndio WAFALME WA MSITU, sifa za kuendelea kiuchumu na kijamii, kunawafanya waanze kuwapanda watu vichwani.
Unajua mikwara yote hii ya Wachina ni propaganda zao wakiamini wataipiga Japan na kuiharibia uchumi wake.