Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,610
Watu wabishi, watakomaa hadi kieleweke...Walishaambiwa atakayebaki mpaka mwezi wa kumi na mbili huko jijini basi yeye mwanaume!
....Ila hawa jamaa kwa kuimba na kumiliki jukwaa nawakubali sana aisee.Muziki wa bendi hasa hizi zenye mahadhi ya kikongo aseee wana hali mbaya sana
Msanii wa filamu nchini na Rais mpya wa FM Academia, Patcho Mwamba amefunguka kwa kusema haoni tatizo kwa bendi za muziki kutumbuiza katika kumbi za baa kwa kiingilio cha vinywaji kwa kuwa wanachoangalia ni pesa wanazolipwa.
Pacho ameeleza hayo kwenye eNewz ya EATV baada ya kuwepo na dhana kwa kipindi kirefu kuwa bendi zikiwa zinatumbuiza ni kujishusha hadhi kwa kuwa kiingilio chake kinakuwa ni kidogo mno huku wengine huweka vinywaji kama kiingilio getini.
"Nakwambiaje bendi ni kama daladala, tunahitaji mtu yeyote apande haijalishi ni mwehu, jini, mchawi, kinachoangaliwa ni nauli yetu tu"alisema Patcho.
Pamoja na hayo, Patcho aliendelea kwa kusema "Tumetoka juzi kwenye mbio za mwenge hakukuwa na kiingilio tulilipwa chetu tukaenda kwenye kukimbiza mwenge, kampeni zikifika watu wanaendaga bila ya kulipia kiingilio. Brand haiwezi kuuliwa kwa masuala ya vinywaji ni upotofu, sisi tukishakodiwa na tukipewa pesa yetu tunaenda kupiga hata kama chooni tutapiga si tumeshalipwa" alisisitiza Patcho.
Kusema kweli Patcho si mwanamuziki wala mcheza filamu ,hizi fani analazimisha tu sababu ya kuganga njaa na amshukuru marehemu Kanumba aliyekuwa anambeba tu,na kwenye muziki kazi yake akipanda jukwaani ni kutaja tu majina ya mapedeshee ili adakishwe kitu kidogo,hakuna cha muziki wala filamu hapo.
Chanzo; EATV
Waliambiwa na nani?Walishaambiwa atakayebaki mpaka mwezi wa kumi na mbili huko jijini basi yeye mwanaume!
Patcho unachofanya sio billionea papa lemutuz hamumtaji kwenye nyimbo zenu au hatoi kitu