Tumelaaniwa na nani????

jonaleemanson

Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
73
Reaction score
70
Tuna mambo ya msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu na watanzania kwa ujumla ambayo tunapaswa kuyajadili lakini tatizo naliona kuna watu kazi yao kukwepesha hoja za msingi kwa watanzania badala yake wanataka tujadili nonsense.

Hakuna asiejua kama kuna shule zimekosa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano kwa matokeo ya hovyo ya kidato cha nne, kulikua na haja ya kuanzisha kitengo cha presidential delivery unity na kukipa bilioni 29 kweli?

Hatuna shida ya umeme na maji mijini na vijijini? Hakuna watu wenye jukumu la kuhakikisha miradi yote inatekelezwa mpaka tuanzishe pdu?hivi viongozi wetu kweli wana nia ya dhati kwa watanzania?

Ushauri kwa watanzania tusikubali kuondoshwa kwenye hoja za msingi kwa mustakabali wa nchi yetu na kizazi kijacho na wahuni wachache wanaofaidika na muundo wakiutendaji uliopo. Tujiulize nani ametuloga jamani?
 
Mchawi wetu ni ccm.. na lile zindiko la bagamoyo ndo kabisaaa...
 
Hamna kurogwa wala nini...ni uvivu na uoga wa kufanya maamuzi magumu huku tukiiacha siasa kufikiri na kufanya kwa niaba yetu

Tuchukue maamuzi magumu..."kitu kitabaki kama kilivyo au katika uelekeo wake mpaka kitakapo pata msukumo kutoka nje"...wa nje ni mimi,wewe na yule...kwa umoja wetu ama mmoja mmoja je tumeanza? ???!!!!!!
 
Ukiwa na asilimia kubwa ya viongozi wanao penda mipasho na kupiga deals unategemea nini? viongozi serikalini wameshindwa kuisimamia na hivyo wamezalisha an idle work force.karibu wizara zote hakuna ufanisi.pamoja na mapungufu ya waziwazi ya baadhi ya viongozi lakini wapo tu wanakula mshahara.pale wizara ya elimu ndio mtihani, kuna uzembe wa kufa mtu.ni kama hawana vision.wanaiongoza wizara kwa kadiri matukio yanavyo kuja.Huko polisi ndio usiseme. hakuna kesi walio wahi kumaliza upelelezi kwao wao adui yao ni CHADEMA! Mwisho wa kufikiri.hata wakiambiwa na mwigulu C.H.U.P.I. siku hizi zina valiwa kichwani, watavaa! si wameambiwa na mkubwa sana anae pita ukubwa wenyewe!kama madawa ya kulevya kg 150 yamepita hapo airport Dar, tuna polisi kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…