usione ndege kuruka ukadhani ananyumba,
usione mbwa kubwika ukadhani ananyumba,
usione kuku kuwika ukafikiri aimba,
usone nguo kunuka ukadhani ya mtumb
usione kuwa na paka ukahisi una samba,
kila unachotazama usione ukadhani
usione jicho kuona ukadhani latazama,
usione mbuzi kunona ukafikiri mzima,
usione mtu kunena ukamuhisi ni mwema,
usione kila cha jana ukafikiri cha nyuma,
usione panapotuna ukadhani pamesoma,
kila unachotazama usione ukadhani,
usione mtu kuchuma ukafiri kuiba,
usione wat kulima ukadhani wanashiba
sione penye huruma ukahisi pana tiba,
usione pepo kuvuma ukafikiri dhorba,
usione panapochoma ukadhani pana mwiba,
kila unachotazama usione ukadhani
cc:
Charles Mloka