Tujikumbushe kuhusu abiria wa ndege ya Air Force flight 571 walioishi siku 72 kwa kula maiti za abiria wenzao

Nilipokuwa nasoma kichwa cha uzi nikadhani ni Infantry Soldier
 
Huu Uzi haujakamilika,maana unamaswali mengi kuliko story yenyewe.
Mosi.je hao wahanga walikula nyama mbichi au iliyochomwa?

Pili,je hiyo mizoga haikuoza mpaka siku72?
Tatu,je hili karatasi La ujumbe walilikuta wapi?
nadhani barafu ndo ilikuwa freezer
 
 
wanatafunaje nyamba mbichi hadi washibe maana hata ukijaribu ya ng'ombe mbichi huwezi kushiba utaishia kutapika
Walijikaza hivyo hivyo ingawa kuna wengine waligoma na kukubali kufa kwa njaa. Aisee , sio poa kabisa.
 
Kama unaweza jaribu hata kuangalia kwenye machapisho mbalimbali kuhusu huo mkasa wameelezea vizuri. Ila kwa kifupi ile ndege baada ya kugonga mlima na kuanguka kuna kipande ambacho kilibaki kwa maana cabin fulani hivi ambacho hiko ndio kwa kiasi kikubwa kiliwasaidia kuwahifadhi na kuwakinga na barafu.

Na humo ndipo walipopata baadhj ya vitu kama hizo peni na karatasi kutoka kwenye mabegi yaliyosalimika. Hata kabla hawajaanza kula wenzao, walikuwa wanakula chocolate walizozipata humo humo kwenye mizigo.
 
Watu wamepitia tabu asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…