Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,493
- 12,461
Kwa hio mkuu wa kaya alifanyiwa hicho kipimo?Wana Jamii Forum wenzangu, ninawasihii tufanye check up za afya mara kwa mara, yaani Physical Check-Up. Hapa USA tunafanya kila mwaka. Kama kuna tatitzo la afya wanaweza kuwahi kutibu kabla hali haijawa mbaya hadi kutishia maisha yako.
Nimeshituka sana kuona Rais wetu mepndwa JK, ameletwa hadi USA kufanyiwa surgery ya Prostate. Nafahamu wengi waliofanyiwa prostate surgery Tanzania na wanaendelea vizuri tu. Lazima hali ya mheshimiwa ilikuwa si nzuri. Labda kachelewa.
Kupima Prostate inabidi daktari aingize kidole huko nyuma kwenye (anus).. Najua wengi hatufurahia hiyo. Na fikiria, unamtia kidole Rais. :A S 13:
Na kwa akina dada uke lazima upimwe kuhakikisha hakuna kasoro kama kansa pia. Nao wanaigiza vyuma huko kucheki Kizazi.
Kazi ipo wenzangu! Lakini ili tuishi maisha mazuri enye afya ni bora tukapime!
nna swali .. PastorPetro
hii kitu ina sababishwa na nini hadi inamtokea mtu, mfano kama mheshimiwa wetu huyo?
Mwanaume yeyote anaweza kuumwa. Ila kuna genetic factors, yaani umerithi nini kutoka kwa wazazi wako. Kama ndugu zako waliugua huenda na wewe utaugua pia. Lakini zamani tulikuwa tunsema mtu kalogwa bila kujua anaumwa nini hasa.:A S-omg:
Pamoja na maelezo na ushauri mzuri wa mleta mada,hoja je ni kweli hakuna vipimo vingine zaidi ya kutiana vidole.?
Heee....!! Hili zito la mwaka, huumwi then uende hospitali umwambie dokta akupime prostate duuh!!
Dalili za ushoga maana utapigwa finga kila mwaka teh teh teh
mtoa mada, asante kwa ushauri, ila naomba kusaidiwa mambo yafuatayo kama utayaweza.
1.kwanza ugonjwa kama huu ulio msumbua mheshimiwa rais, unasababishwa na nini?
2.Pili ni dalili gani mgonjwa anaweza kuzipata akiwa na ugonjwa huo?
3.Mwisho ungonjwa huo ni mbaya sana kiasi kwamba mtu akizembea unaweza kuleta madhala makubwa? na kama ni ndio ni madhala gani? tatizo uku bongo siasa nyingi habari za afya zetu hatuzingatii sana!!
Wana Jamii Forum wenzangu, ninawasihii tufanye check up za afya mara kwa mara, yaani Physical Check-Up. Hapa USA tunafanya kila mwaka. Kama kuna tatitzo la afya wanaweza kuwahi kutibu kabla hali haijawa mbaya hadi kutishia maisha yako.
Nimeshituka sana kuona Rais wetu mepndwa JK, ameletwa hadi USA kufanyiwa surgery ya Prostate. Nafahamu wengi waliofanyiwa prostate surgery Tanzania na wanaendelea vizuri tu. Lazima hali ya mheshimiwa ilikuwa si nzuri. Labda kachelewa.
Kupima Prostate inabidi daktari aingize kidole huko nyuma kwenye (anus). Najua wengi hatufurahia hiyo. Na fikiria, unamtia kidole Rais. :A S 13:
Na kwa akina dada uke lazima upimwe kuhakikisha hakuna kasoro kama kansa pia. Nao wanaigiza vyuma huko kucheki Kizazi.
Kazi ipo wenzangu! Lakini ili tuishi maisha mazuri enye afya ni bora tukapime!
Kipimo hicho hakiepukiki unapopata shida kama hiyo.Kwa hio mkuu wa kaya alifanyiwa hicho kipimo?
Hata wewe Unaweza kufanyiwa kafanye checkup mara moja kabla kidole hakijakuhusu.Kwa hio mkuu wa kaya alifanyiwa hicho kipimo?
Kama huamini subiri uumwe!Hii ni kampeni ya ushoga tu sio bure pastor mzima unaleta mada kama hii? utakuwa unalipwa wewe.
Kwa niaba ya mtoa mada nitajibu maswali yako hapo juu.
1. Kwanza ugonjwa wenyewe unaitwa BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH),i.e. an enlargement of the prostate gland (kuvimba au kuongezeka kwa tezi ya kibofu.
-Sababu (causes) mara nyingi haijulikani,ingawa unawezakusababishwa na mabadiliko ya homoni (androgens) inayoenda sambamba na utu uzima (hasa kati ya miaka 50+...)
2. Dalili anazowezakuzipata mgonjwa:
-Urine retention (kushindwa kukojoa) sababu uvimbe huwa unaziba njia ya mkojo
-Nocturia (kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku)
-Kuhisi kama mkojo haujaisha kwenye kibofu baada ya kujisaidia (sensation that the bladder has not completed emptied).
-Anaweza kupata U.T.I sababu ya urine stasis
-Anaweza kupata hata hydronephrosis (Matatizo ya figo) n.k
Hizo ni baadhi ya dalili ambazo ni common,lakini kwakweli zipo nyingi.
3.Sasa madhala kama mtu akizembea ni pamoja na hilo nilisema hapo juu,yaani Hydronephrosis.
-Mengine ni kama uharibifu (damage) wa kibofu cha mkojo,muscles zinalegea hata kushindwa ku-control flow ya mkojo kutokana na pressure inayoongezeka kwa sababu ya mkojo kushindwa kutoka.
-U.T.I n.k
Nadhani umenielewa kidogo mkuu.
Hii ni kampeni ya ushoga tu sio bure pastor mzima unaleta mada kama hii? utakuwa unalipwa wewe.
Hata wewe Unaweza kufanyiwa kafanye checkup mara moja kabla kidole hakijakuhusu.
Ukitaka kujiwa ustaarab wa jamii fulani basi fuatilia mijadala yao. Hii mada imevuka mipaka na kukosa ustaarab kabisa.
MODs, Mhariri tafadhali naomba muifute.
kweli unatujali mkuu endelea kutupa dataHakuna aliyenilipa kuposti kitu hapa. Ninawajali sana watanzania wenzangu. Nasikitika kuwa watu wanaugua na kufa kwa sababu wanaogopa kufuatilia afya zao. Mwenyezi mungu akubariki.