Trump amekalia kuti kavu

Lavan Island

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2015
Posts
2,378
Reaction score
2,057
Bw. Trump anataka kujua ni nani aliyempatia taarifa mfichua siri huyo,akiongeza kuwa aliyefanya hivyo ''anakaribia kuwa jasusi".

Trump anashutumiwa kwa kutafuta msaada kutoka nchi ya kigeni kwa minajili ya kumchafua kisiasa mpinzani wake Joe Biden na kutumia msaada wa kijeshi kama nyenzo ya kutaka matakwa yake yatimizwe.

Bw Biden ndiye kinara wa mbio za tiketi ya kugombea urais 2020 kwa chama cha Democrats.

Haki miliki ya pichaEPA
Bwana Trump amekiri kuwa alimzungumzia Joe Biden na Bwana Zelensky, na kuwa alizuia msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo wa thamani ya dola milioni 400.

Lakini amekanusha kuwa alifanya hivyo kama shinikizo kwa Ukraine ili kumchunguza Biden.

Mfichua siri ni nani?

Hakuna taarifa za kina kumhusu lakini wakili wake ameonya kuwa jaribio la kubaini ni nani litamweka hatarini.

Magazeti ya New York Times, Washington Post, na shirika la habari la Reuters yanadai kuwa mfichua siri huyo ni afisa wa CIA.

Mazungumzo baina ya Trump na Zelensky yalikuwaje?
Kwa mujibu wa mukhtasari uliotolewa jana na Ikulu ya White House, Trump alimwambia Zelensky juu ya namna ambavyo Joe Biden akiwa makamu wa rais alishawishi Ukraine kumtimua kazi mwendesha mashtaka wake mkuu, Viktor Shokin mwaka 2016.

Ofisi ya Shokin ilifungua jalada la uchunguzi dhidi ya Burisma, kampuni ya gesi asili ambayo mwana wa Joe Biden, Hunter alikuwa ni mjumbe wa bodi yake.

Nchi kadhaa za magharibi pia zilikuwa zikishinikiza Bw Shokin atimuliwe kazi kwa madai alikuwa akivumilia vitendo vya rushwa.

"Nimesikia mlikuwa na mwendesha mashtaka ambaye alikuwa ni mzuri kweli na alifutwa kazi kwa njia ya uonevu. Watu wengi wanalizungumzia jambo hilo," Trump ananukuliwa akisem kwenye mazungumzo hayo na kuongeza: "Kitu kingine, kuna mjadala mkubwa kumhusu mtoto wa Biden, kuwa baba yake alizuia waendesha mashtaka na watu wengi wanataka kujua undani wa hilo, so chochote unachoweza kufanya na Mwanasheria Mkuu (wa Marekani) litakuwa jambo jema.

"Biden alikuwa akijitamba kuwa amezuia uchunguzi angalia utakachokifanya hapo...ni jambo baya sana kwangu."

Zelensky anaripotiwa kujibu: "Tutalishughulikia hilo na tutafanyia kazi uchunguzi wa kesi hiyo.

"Juu ya hilo, pia ningeomba kama una taarifa zozote za ziada pia tupatie, zitatusaidia sana."

Akimshukuru Trump, bw Zelensky alisema kuwa alikaa kwenye jumba lake la jijini New York, Trump Tower, mara ya mwisho alipozuru nchini humo.

Zelensky amesema nini?
Haki miliki ya pichaEPA
Image caption
Bw Zelensky na Trump wamekutana Jumatano jijini New York Jumatano
Raisi huyo wa Ukraine amesema alidhani kuwa maelezo ya Trump pekee katika mawasiliano hayo ndiyo ambayo yangechapishwa.

"Nadhani, wakati mwengine, mawasiliano ya simu baina ya marais wa nchi huru hayatakiwi kuchapishwa," Zelensky ameviambia vyombo vya habari vya Ukraine akiwa jijini New York, kwa mijubu wa shirika la habari la kimataifa la Reuters.

Bw Zelensky ameongeza kuwa kesi ya Hunter Biden ni miongoni mwa kesi nyingi ambazo huwa anazijadili na viongozi wa kimataifa.

"Kwangu mie, hii ni moja ya kesi nyingi ambazo huwa nazifanyia mazungumzo na viongozi wa mataifa mengine, endapo wananiuliza," ameeleza raisi huyo.

"Wakati mwengine, kesi hizi huchunguzwa ama huwa hazijachunguzwa kwa muda mrefu - na sijui kwanini," ameeleza.
SOURCE;BBC
 
๐Ÿ˜ต๐Ÿ˜‰Zelensky Rais mchekeshaji atakuwa ameianza kazi halisi ya urais kwa kusababisha Rais wa taifa kubwa kama Marekani kuingia matatani. Jambo la kujiuliza ni Je Trump alimuona Zelensky wa kuja na kumwona kama ngazi ya kupandia au Zelensky alimuona Trump kama boya na mtelemko wa kuisaidia Ukraine ipate kuungwa mkono kimataifa?..... Muda utaongea hivi karibuni.
 
Mazungumzo ta Trump ni wazi yalitaka kitu cha zaidi kitakachomsaidia kupata pointi za kummaliza Biden. Ila Trump ni kichwa maji na mtata sana. Sijui watamtoaje. Huyu Trump hata ikithibitika kuwa alibaka atajaribu kupindisha mambo kuwa ubakaji huo ni ajenda za WITCH HUNT za wapinzani wa Democratic Party.
 
Haijalishi na Biden nae wakisema kila kitu kinyoke kama inavyotakiwa kwenye suala hilo anajipaka matope....Dems wanatakiwa waandae mtu 2024,mtu sahihi wa kupambana na mwingine wa Reps.Kwa sasa wakae kitako tu.
 
Nilivyosoma hiki kipande nilishtuka sana,kumbe Waziri wa Mambo ya Nje ana nguvu sana
 

Wanamtafitia Trump umaarufu hakuna lolote. Impeachment haitafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ