nakuunga mkono ndugu yangu nami boda boda langu limekutana na kadhia hiyo hapo moroNipo Morogoro na nimebahatika kuangalia Abood TV asubuhi na kukutana na kituko hiki.
TRA wanakusanya kodi kwa waendesha bodaboda na kijana mmoja aliyekuwa akiwakimbia alifukuzwa na gari la TRA na kutumbukizwa mtaroni kisha gari lile likakimbia.
Mku wa TRA anaeleza kuwa watu watii sheria za nchi akijitahidi kutetea kitendo hicho.
Je TRA wanruhusiwa kufanya haya?
Nimeliweka jambo katika siasa kwani juzi tu hapa Masasi kulichafuka na kuitia serikali hasara kwa upuuzi wa trafiki mmoja aitwae Komba.
TRA tafuteni njoa mbadala za kuwabana bodaboda kuliko kufukuzana nao barabarani,nchi ina watu ambao wamekata tamaa na wanaweza wakatutia katika doa kwa jambo dogo.
1. Nyie wamiliki wa bodaboda mmewafundisha madereva wenu maadili ya kuendesha hizo pikipiki barabarani, huo ni ujinga wa dereva wako kujichukulia sheria mkononi, si angesimama na kupewa maelekezo.
2. Mnajua hizo kadhia wanazosababisha pindi ikitokea ajali hata kama wanamakosa.ni vifo vingapi wamesababisha pindi wakumbwapo na ajali. acha kusahabikia ujinga wa madereva wa bodaboda!
Umekuwa nje ya maada lakini si kitu ngoja tujaribu tena.Suala kubwa ni kuwa TRA wan haki ya kumgonga mtu kwa kuwa kawakimbia?1. Nyie wamiliki wa bodaboda mmewafundisha madereva wenu maadili ya kuendesha hizo pikipiki barabarani, huo ni ujinga wa dereva wako kujichukulia sheria mkononi, si angesimama na kupewa maelekezo.
2. Mnajua hizo kadhia wanazosababisha pindi ikitokea ajali hata kama wanamakosa.ni vifo vingapi wamesababisha pindi wakumbwapo na ajali. acha kusahabikia ujinga wa madereva wa bodaboda!
hapo kwenye red mkuu! hiyo idara kwa mujibu ya tra act ya mwaka 1996 iliyoanzisha mamlaka! inatakiwa ifanywe na customs department! ila kwa uroho wa tra watu wa domestic revenue mbao ndio tupo nao wengi huku wilayani! wanawatishia mpaka bastola wafanyabiashara iliwatoe kodi!TRA wana kitengo cha Enforcement and Compliance kwa watu makaidi kama hao wa bodaboda kwani wakati anakimbia hakujua kama atapata ajali? kama angekuwa hana kosa alikuwa anakimbia nini?
Sidhani kama uko Tanzania hii inayoelezewa hapa ni kweli ziko wazi lakini suala ni nani anazisimamia ili zitende haki.Dunia kote raia wanalipa kodi kwa serikali zao kwa hiari pale tu wanapoona haki inatendeka.Haiwezekani watu na Makampuni yenye uwezo wa kulipa kodi wapewe Misamaha isiyoelezeka halafu Mamlaka za kukusanya kodi ziingie barabarani kufukuzana na waendesha Pikipiki.siungani nawe, sheria ziko wazi..kama kila mtu atakimbia hao tra wataitoa wapi hiyo kodi, tatizo hapa si madereva tu bali hata wamiliki..tutii sheria