Tofauti ya Ct Scan na MRI

CT scan au computer tomography inatumia mionzi ya xray kutengeneza picha ya mgonjwa na kuitupia kwenye screen kwa ajili ya radiologist kutafsiri.
MRI au magnetic resonance imaging inatumia mawimbi ya radio, ie radio waves na sumaku kutengenza picha ya eneo husika la mgonjwa na kuzitupia kwenye kompyuta kwa ajili ya kuangalia

Hizi mambo zina maelezo mengi, kwa kifupi na uelewa wa kawaida ni hivyo.
 
Kwaiyo zote zinafanya kazi moja? Au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu naomba kuelimishwa utofauti wa CT scan na MRI

Kuongezea tu hapo kwa mchangiaji ambae literally ametoa tofauti za kiteknolojia.
Katika Matumiz, MRI inaweza kuonesha mpaka soft tissue, wakati CT scan kwa sababu inatumia teknolojia ya Xray haioneshi zile soft tissue, inaonesha zile denser tissues.
Kwa mfano katikati ya pingili za mgongo huwa kuna Disc, ambayo ni mfumo wa cartilage(nyama ngumu mithili ya ile ya sikio au pua)
CT scan itaonesha ile mifupa ya mgongo tu ila MRI itaonesha vizuri zaidi, disc mpaka spinal cord.
Mfano mwingine ni ukipata injury ya goti ukakatika Tendons(Kwa mfano wa nyama ya ng'ombe ni ile kitu nyeupe mithiri ya Mpira na haitafuniki), MRI ndo kipimo superior sababu tendon inakua much softer
Kwa CT scan kuona tissues kama hizo inakua ngumu ila kwa MRI inakua rahisi zaidi.
Kila kipimo kina mipaka yake na use cases zake, unaweza kufanya CT scan ukaambiwa urudie kufanya MRI, usichangae siku ikitokea.

Nafikiri nimejitaidi kutumia layman's language na nimeeleweka
 
Asante sana Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…