Wakuu nauliza kwa mliojenga tayari, Ulitumia Tofali ngapi kujenga msingi tu wa nyumba yenye vyumba 3 ikiwa na jiko dining na public toilet! Na je gharama gani inafaa kumlipa fundi kwa ujenzi wa msingi tu?. Eneo la kiwanja ni flat tu hakuna slope.
Mkuu swali lako lingejibika vizuri Kama ungeweka ramani na eneo lako Kama Ni tambarare au Lina muinuko mfano nikuulize toka dar Hadi Kilimanjaro gari itakula mafuta kiasi gani bila kutaja aina ya gari
Mkuu swali lako lingejibika vizuri Kama ungeweka ramani na eneo lako Kama Ni tambarare au Lina muinuko mfano nikuulize toka dar Hadi Kilimanjaro gari itakula mafuta kiasi gani bila kutaja aina ya gari
Ndo hivyo mkuu hapo akili nayoweza kukupa kwa Ni tafuta mafundi wa tatu tofauti kila mtu akupe makadirio yake alafu chukuwa yule mwenye Bei ndogo ila hakikisha hao mafundi Ni kutoka maeneo tofauti ila tofali lazima zicheze kwenye 1500 Kama ulipo Kuna mawe Bora ujenge msingi wa mawe
pima mzingo wanyumba yako kwa futi(urefu jumlisha upana)kuta zote.
ukishapata kadiria au amua ni togfali kisi gani unataka msingi wako unyanyuke zingatia msingi mfupi sana kama bado tanroad au tarura hawajaweka barabara hapo unapojenga lazima watajaza kifusi na kama msingi wako utakuwa chini kuliko kifuis chao jua unatengeneza bwawa jaribu kunyanyua uwezavyo.
Upipata mzingo wako sasa mfano ni ft 1000 za mzingo gawanya kwa tofali moja lina ft1.5 utapata tofali karinia 666 kwa mzunguko mmoja sasa unataka kupandisha kozi ngapi au tofali ngapi zidisha mf; 666*3=tofali 2000.
pima mzingo wanyumba yako kwa futi(urefu jumlisha upana)kuta zote...ukishapata kadiria au amua ni togfali kisi gani unataka msingi wako unyanyuke zingatia msingi mfupi sana kama bado tanroad au tarura hawajaweka barabara hapo unapojenga lazima watajaza kifusi na kama msingi wako utakuwa chini kuliko kifuis chao jua unatengeneza bwawa jaribu kunyanyua uwezavyo... upipata mzingo wako sasa mfano ni ft 1000 za mzingo gawanya kwa tofali moja lina ft1.5 utapata tofali karinia 666 kwa mzunguko mmoja sasa unataka kupandisha kozi ngapi au tofali ngapi zidisha mf; 666*3=tofali 2000.........
Ni kweli ila inaweza na ugeni wa haya mambo ndo maana ila nadhani Bora atafutr fundi was huko huko aliko huu ushauri wa mtandaoni unataka mtu mwenye A, B, C za ujenzi angalau kidogo