TMK Majita - Tunadatishe

Joined
Nov 8, 2018
Posts
23
Reaction score
27
TMK MAJITA - FIRST BORN LB GENIUS "TUNADATISHA"

Unachonizidi ni promo/
Usijiite mkali zaidi yangu/
Ujiulize, ingekuwa vipi meneja wako angekuwa wangu?/
Umahiri wa mashairi ndio kisa unajenga beef/
Wana-diss level ndogo, eti mistari so nadhifu/
Maadui wameshamili, kuona sasa Muziki dili/
Wako data chuga skendo, promota akunyime dili/

Yaani kipaji changu ndio kimejenga uadui/
Hata mchaga wameshaulapa, wakiapa kujeruhi/
Naifanya hii sanaa kwa uwezo wa Mungu mpaka kufa/
Kwa tungo zenye akili, mpumbavu anionyeshe nyufa/
Vina vyangu nakaza, najua kesho itakufaje/
Kwenye beef isiyo na faida, sina muda wa kupoteza/
Majita kama meli, haizami kwa uzito wa nanga/

Kipaji tuna uwezo, haina support kama mganga/
Nasema ila asichokoze kilichosemwa kwenye ugomvi/
Utashindwa kuoga mtoni kama mwanaume mwenye govi/
Ni fataki tu za vina, mpaka adui akikwe gome /
MC usinipata, saka darasa ukasome/
Level sio upepo wa feni, ni kimbunga cha katrina/
Nikivuma, nang'oa vyote toka tawi mpaka shina..

UKWAJU WA KITAMBO
0767 542 202



Rest in Peace lb genius the first born
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…