Timu yangu Simba yasuasua

Udaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2012
Posts
724
Reaction score
109
Washabiki wenzangu hebu tujadili hili tumecheza mechi 4 nakuambulia point4 ingawa hatujafanikiwa kupoteza bado lakini tukumbuke tayali tumepoteza point8 hadi sasa katka michezo minne ambayo tayali tumeshacheza alafu kikubwa zaidi michezo tumecheza nyumbani ingawa leo tulikuwa niwagen wa watani zetu lakn bado tulikua palepale taifa,mm binafsi inaniuzunisha naomba tujadili.
 
Laana ya Michael wambura,imeanza na ndumbaro,bora aveva atafute muafaka
 
sijui..labda uwaulize simba ukawa
 
Simba tuko vizuri kwa TZ hii cc wenyeji kokote tunauwezo wa kushinda, tofauti ya anayeongoza na cc ni ndogo sana USIHOFU
 
Simba tuko vizuri kwa TZ hii cc wenyeji kokote tunauwezo wa kushinda, tofauti ya anayeongoza na cc ni ndogo sana USIHOFU
Mkuu kweli? maana jana hali yangu ilikuwa mbaya sana ,tungefungwa nahisi mke wangu angekuwa mjane sasa!
 
Mkuu kweli? maana jana hali yangu ilikuwa mbaya sana ,tungefungwa nahisi mke wangu angekuwa mjane sasa!

Mimi nilipata hofu zaidi pale yule dogo wakibrazil alipo miliki mpira kati yamabeki nakupiga tik taka mungu alikua nasi pale tungelia.
 
Mimi nilipata hofu zaidi pale yule dogo wakibrazil alipo miliki mpira kati yamabeki nakupiga tik taka mungu alikua nasi pale tungelia.

Mie hiyo sare tu nimeipa bonge la "phew!" yaani bora nifungwe na yeyote kuliko huyu funza wa kijani njano!
 
Hizi timu za Yanga na Simba zinahitaji kujiangalia zaidi, majina ya timu ndiyo yanalazimisha umaarufu zaidi ya uwezo wa kucheza uwanjani. Bila mabadiliko makubwa umaarufu utaendelea kukuzwa na vyombo vya habari lakini siyo uwezo uwanjani
 
Mie hiyo sare tu nimeipa bonge la "phew!" yaani bora nifungwe na yeyote kuliko huyu funza wa kijani njano!

Ni kweli! Sasa nendeni kaitaba, Turian nk mkafungwe halafu mkiwa nafas ya 7 mulaum wakati mnataka wenyewe.
 
Kumbeeee, ndo maana mashabiki wa simba walifurahi sana wakati wale wa YANGA wakiwa na huzuni, hapa sasa napata jibu..
 

Kuwa Mvumilivu Kujenga Timu Kunahitaji Moyo wa CHUMA. Sasa Hivi UTAIKUBALI SIMBA!
 
GENTAMYCINE kumbe na wewe ni wavumilivu fc,unafaa kuwa fan wa arsenal lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…