Mechi kati ya Manchester na Chelsea itakuwa ngumu sana ingawa Manchester watashinda kwa magoli mengi 3 au 4.Manchester wako vizuri kuanzia nyuma katikati na mbele.Kipa wa Manchester David alianza vibaya lakini mechi tatu za mwisho Spurs ,Arsenal na Bolton ameonyesha uwezo mkubwa sana.Upande wa beki Manchester wako poa sana kuumia kwa Rio na Nemanja hakukuathiri ngome yao.Mwaka jana sehemu ya kiungo ilipwaya sana lakini mwaka huu Anderson na Clevely wamekamata barabara sehemu ya kiungo.Ushambuliaji ni balaa John Terry na safu nzima ya ulinzi ya Chalsea watapata wakati mgumu sana kuikabili safu ya ushambuliaji ya Manchester United ikiongozwa na Rooney,Chicharito,Young na Nani.