[TABLE="width: 650, align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"]ATUDO: Jembe jipya ndani ya Azam[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #FFFFFF, align: left"] [TABLE="width: 51%, align: left"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: mwanacss, bgcolor: #B47C01, align: left"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
DORIS MALIYAGA
LIGI Kuu Bara ina mabeki wengi, lakini Mkenya wa Azam FC, Jockins Otieno Atudo anatofautiana nao kwa mambo kadhaa.
Amejengeka kimazoezi na ana mwili mkubwa ambao unabebwa na kipaji kuhimili nafasi yake ya beki wa kati. Ni beki mwenye uwezo wa kipekee wa kulinda timu yake na mara kadhaa kupachika mabao.
Kimuonekano ni mweusi, mrefu na ana umbo lililojengeka na mkakamavu. Ni miongoni mwa mabeki waliosainiwa na kocha Mwingereza Hall Stewart kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
Alitua Azam FC akitokea Tusker ya Kenya na amekuwa mstari wa mbele kuimarisha ukuta wa Azam akishirikiana kwa ukaribu na beki mwenzie David Mwantika.
Katika staili ya uchezaji wake anatumia zaidi akili na nguvu hali inayowafanya mastraika wasumbufu washindwe kumpenya.
Atudo ni mzuri katika kufunga mabao ya kichwa.
Panapotokea mipira ya adhabu yoyote kama kona na krosi lazima uwe makini naye.
Tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo kwa ajili ya mzunguko wa pili tayari amewafungia mabao sita katika michuano mbalimbali.
Kati ya mabao hayo moja amefunga kwenye ligi mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, matatu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi wakawa mabingwa na mawili walipokuwa kwenye mashindano ya Kombe la Hisani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako walitwaa ubingwa.
"Sababu ya kufanya vizuri ni kutambua majukumu yangu katika kazi, kujituma na ushirikiano wangu na wenzangu," anasema Atudo anayevutiwa na soka la Thomas Vermaelen beki wa kati wa Arsenal na Ubelgiji.
"Napenda kujifunza kila siku na kufuata maelekezo ya yoyote nitakayopewa na kocha. Uwepo wangu Azam nimevutiwa na mipango ya timu,"anasema Atudo ambaye pia ni shabiki wa Arsenal.
"Baada ya kucheza nyumbani kwa kipindi kirefu, nimeona nitoke kwa ajili ya kutafuta njia nyingine ya mafanikio, unajua unapocheza nyumbani tu hupati changamoto kama unapotoka na kuja sehemu kama Tanzania."
"Tangu nimefika maazimio yetu ni kutwaa ubingwa wa ligi jambo ambalo tutalikamilisha lakini pia tunataka kuweka historia katika michuano ya kimataifa kutokana na kiwango cha juu tutakavyokionyesha,"alisisitiza.
Anavyoizungumzia Azam
"Azam ni timu nzuri na ina ushindani wa hali ya juu. Ushindani uliopo ni baina ya wachezaji wenyewe kwa wenyewe kila mmoja akitafuta namba ya kucheza,"anasema Atudo.
"Sina uzoefu na timu hii lakini nimeona wapo wachezaji wazuri wenye bidii na heshima wanaoweza kuipeleka Azam mahali popote. Nimegundua hili kwa mara ya kwanza nilipofika kwani pamoja na ugeni wangu sikuhisi tofauti na niliishi kama mwenyeji,"anasisitiza Atudo.
Kuhusu michuano ya kimatifa na mechi za ligi, Atudo anasema klabu yao itafanya vizuri kwa sababu maandalizi ni mazuri.
"Azam ni wageni katika michuano ya kimataifa lakini mategemeo yangu tutafanya maajabu msimu huu kwa sababu maandalizi tunayofanya ni mazuri.
"Na si michuano hiyo tu hata kwenye ligi mambo yatakuwa mazuri,"anasisitiza mchezaji huyo, ambaye timu yake sasa ipo raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho.
Tofauti ya Kenya na Tanzania
"Mpira wa Kenya na Tanzania ni tofauti hasa katika uchezaji. Mpira wa Kenya ni nguvu na vurugu hupati nafasi ya kutamba kirahisi, lakini Tanzania si sana,"anasema Atudo.
"Mpira wa Tanzania mwepesi na una kasi hata hivyo nimeshakuwa mzoefu sasa."
Nje ya soka
"Natumia muda wangu mwingi kukaa na familia yangu nyumbani hata hapa Tanzania huwa natulia tu nyumbani, sipendi kuzunguka bila sababu."
Atudo anasema kitu kinachomvutia zaidi Tanzania ni ukarimu wa wenyeji: "Watanzania ni wakarimu na watu wa kusaidiana katika maisha yote tofauti na sehemu nyingine."
Historia
Kipaji chake cha soka tangu akiwa mdogo na alianza kufanya vizuri shule ya msingi alikuwa anasoma Sonny. Umaarufu wake uliongezeka zaidi akiwa Sekondari ya Pe-hill alikosoma hadi kidato cha nne.
Pamoja na kufanya kwake vizuri katika soka lakini Atudo aliona elimu ndiyo jambo muhimu kwake akamua kuendelea na masomo na kusoma kidato cha tano na sita katika sekondari ya Kisumu.
Mara baada ya kumaliza, hapo ndipo Atudo akajiingiza rasmi kucheza soka la ushindani na alisajiliwa na klabu ya Sonny Sugar 2005 kucheza Ligi Kuu.
Akiwa na Sonny aliichezea miaka mitatu akahamia Tusker FC klabu aliyoichezea kwa mafanikio makubwa na muda mrefu kutoka 2008-2012 aliposajiliwa na Azam.
Ujio wake Azam ni baada ya kuonwa na kocha, Stewart Hall akicheza ligi ya Kenya. Hall alikuwa Kenya mara baada ya kuachana na Azam kwa muda akenda kuifundisha Sofapaka ya nchini humo.
Juu ya maisha yake kifamilia, Atudo anasema wako watano na yeye ndiyo wa kwanza. Ndugu zake wengine ni Collins, Midred, Felix, na Zaina ambao wanafanya shughuli zao wenyewe.
Atudo ni baba wa familia yenye mke (hakutaja jina lake) na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa, Neville (1.4).
JOCKINS OTIENO ATUDO
Kuzaliwa: Agosti 8, 1988
Mahali: Migori, Kenya
Klabu: Sonny Sugar 2005-2008,
Tusker 2008-2012, Azam FC 2012-
Taifa: Kenya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
sosi:
ATUDO: Jembe jipya ndani ya Azam