TFF wanaigopa Simba?

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,297
Reaction score
18,053
Sakata la usajili wa Ngasa linaonyesha kuwa TTF hawako makini katika kushughulikia matatizo ya usajili yanayojitokeza mara kwa mara. Sakata la Ngasa kwa kiasi kikubwa linafanana na sakata la Mbuyu Twite msimu uliopita. Pengine hata la Kelvin Yondani. Katika hili la Ngasa na kabla yake Twite, Simba ilifanya makosa ya kutofuata taratibu na kanuni za usajili. Kwa Twite walienda moja kwa moja kwa mchezaji bila kujali ya Club yake ya DRC. Kama Ngasa, alikuwa kwenye mkopo timu nyingine nchini Rwanda. Ngasa naye alikuwa kwenye mkopo Simba akiwa ni mchezaji wa Azam. Walimsainisha akiwa na mkataba na timu ya Azam kinyume cha kanuni. Katika yote hayo mawili, TFF wameamua Simba irudishiwe pesa zake ambazo kwa kweli walizotoa kwa uzembe wao. Kwa Ngasa na faini juu yake.
Cha ajabu kabisa, hakuna adhabu ambayo Simba au kiongozi wa Simba aliyehusika amepata adhabu yoyote. Kwa msingi huo, viongozi wa Simba wataendelea na uhuni wao kama hakutakuwa na adhabu. Ndio maana najiuliza, TFF wanawaopgopa viongozi wa Simba? Kiongozi mmoja akifungiwa japo mwaka, bila shaka watashika adabu na uhuni huu utapungua kama sio kuisha kabisa. Kwa nini Ngasa apate adhabu peke yake wakati kosa limefanyika pande mbili? Kama ilivyo katika rushwa lazima awepo mtoaji na mpokeaji. TFF walifanyie kazi suala hili. Viongozi wa Yanga pia wafuatilie ili haki itendeke na ionekane imetendeka.
 
Hii timu inabidi Ifungiwe usajili miaka miwili au Ishushwe daraja. Pesa zenyewe hawana wanakimbilia wachezaji wazuri wenye majina makubwa barani Afrika kama akina Ngassa. Simba Ishushwe daraja ili ijifunze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…