Tenzi za huba

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,833
Reaction score
3,753
>Moyoni sina amani, kama nchi za kiarabu
>Kifikra nipo utumwani, nafsi inapata adhabu
>Penzi lako kwa hisani, kupata bahati nasibu
>Nakesha madhabahuni, labda utakuja kutubu

>Roho yangu rehani, pumzi nazihesabu
>Siha yangu tafrani, nakuhitaji ewe tabibu
>Nipe tiba yakini, laaziz uvune dhawabu
>kwangu salama salmini, karibu wangu zabibu

>Uzuri ni sura, tabia nitakubadili
>Hekima na busara, nitakufunza hata usijari
>Nitakupa mafunzo bora, ya mila na desturi
>Papara za ukapera, zangu nitazitupa mbali

>Nataka tuwe wachumba, sio dada na kaka
>Nikugande zaidi ya ruba, ama tatoo sio stika
>Nikikuita mahabuba, usisite kuitika
>Nizamishe ndani ya huba, kwa mahaba ya uhakika.......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…