Haya makato uliyotaja si sababu toshelezi kwa huduma kuwa ghali. VAT inategemea ukubwa wa fees na hayo mengine. Hiyo percent ni kubwa mno km transaction charges. Mimi binafsi niliachana na ujinga wa mobile banking hasa unapoenda kwenye mtandao wa simu. Sijui ni dunia ipi transaction charges ni kubwa hivi. Bahati mbaya makampuni ya simu hadi yamehama kwenye core business activities na benki zimeshindwa kujipambanua vilivyo kuweza kushindana. Matokeo yake, usimamizi mbovu wa sekta na huduma ghaliVAPS, hufahamu lolote mkuu, hiyo pesa ina mlolongo sana, ukitathmini kiundani utaona ni ada ndogo
mgawanyo upo hivi
1. ukitoa pesa kwa wakala serikali inachukua 18% as V.A.T kwa hiyo katika hiyo 1450 serikali chao ni 261
2. Wakala aliyekuwekea hiyo pesa anachukua 200
3. wakala atakaekupa hiyo pesa anachukua 300
4. Bado wakala mkuu hajapewa chake
5. Bado benki haijapewa
6. bado mtandao husika haujapewa chake
NB
Mnavyoweka hamkatwi kitu
Sent using Jamii Forums mobile app
VAPS,
Nunua Vocha ya VODA 1000 then jaribu kujiunga kifurushi cha 1000, utaambiwa fedha haitoshi na watakuaambia wa "kupige tafu". Inaamana VODA wakisema kifurushi ni sh 500, 1000, 1500 etc hakimaanishi thamani un less otherwise ununue kwa MPESA ndio inakubali.
Mbaya zaidi Vocha ni za 500, 1000 etc hivyo ukitaka ongeza lazima uongeze kitu kizima yaaani kama unataka kununua kifurushi cha 500 lazima uwe na zaidi ya hela hio. Vile vile bando ya internet ikiisha hawatoi taaarifa mpaka wamekwangua airtime yote iliyobaki... kwa kweli hawa ni wezi kupindukia.....