Dunduliza hela kidogo kidogo uanze kufanya biashara ya mtaji wa chini,mtaji wenyewe uwe kati ya 100,000/= hadi 500,000/=.
Tumia muda wako mwingi sana kufikiria biashara ya kufanya,mambo ya kuajiriwa usifikirie tena.
Kama umeiva kwenye kufundisha somo lolote kwa madogo wa O-level,maana O-level ndiyo kwenye soko kwa sababu O-level ambao ni wateja wenyewe wako wengi sana.
Tafuta dogo yeyote wa O-level anza kumfundisha bure somo moja tu unaloliweza sana,unaweza kumfundisha popote pale,iwe kwako,au chini ya mti,au kwao au hata popote pale ili mradi pawe ambapo hupalipii chochote.Dogo akiona unamfundisha vizuri atakuletea wenziye kibao,hapo ndipo utakapopata mtaji wa kufanyia biashara.