Tanzania hit by second ICSID dispute related to Mining Retention Licenses

Hii kesi tunashindwa tu... ni mara chache sana kwa nchi kushinda kesi zinazofunguliwa huko ISDS dhidi ya nchi husika.. Tujipange kwa sasa maana track record ya mahakama ya ISDC inajulikana sana tu ... hakuna nchi kushinda bali makapumpuni...
Kwa mujibu wa bandiko inaonesha hatujafanya hata effort ya kupambana mahakamani. Utashindaje kama hata hujaonesha kuguswa?
 
Uongozi haujawahi kuwa ni mabavu na majigambo, viongozi someni uongozi wa mfalme Suleiman. Nchi itaangamia kwa ukosefu wa viongozi wenye busara
 
Ofisi ya Attorney general wanaenda front wenyewe? Hawana wanasheria wa nje huko wanaoweza kula sahani moja na Wazungu?
Nafasi ya kushinda ni ndogo, bora kuokoa gharama kwa kutotokea kabisa halafu hukumu ikitoka tukatakiwa kulipa hilo lifidia tunaendelea kupiga danadana hadi wadai wachoke wenyewe kama mkulima wa sauz
 
Kwa mujibu wa bandiko inaonesha hatujafanya hata effort ya kupambana mahakamani. Utashindaje kama hata hujaonesha kuguswa?
Ndugu, fanya tu utafiti na utajua takwimu zinasema nini.. mimi ni mwanasheria huku ng'ambo na nimekwisha simamia kesi kubwa katika the biggest four employers wa dunia hii, hata kabla ya kusoma particulars za kesi hiyo, ninaweza kusema bila kigugumizi na ninakuhakikishia, hatuchomoki... wewe angalia tu ni nchi ngapi zimewahi kushinda hizi kesi za ISDS? Nimekwisha andika machapisho mengi katika jumuia ya kimataifa na hili jambo la ISDS nimekwisha lizungumzia hapa - soma tu hapa na utaona kinachozungumzia hata kabla hatujapelekwa huko ISDS...
"Public-Private Partnerships: No Investment Without An Investor-State Dispute Settlement Or Investment Court System"
Published in Adjuris - Society of Juridical and Administrative Sciences, International Conference: “Perspectives Of Business Law In The Third Millenium” www.Businesslawconference.Ro - Seventh Edition - November 24, 2017.
 
Makada wa "veggies" watatuambia ni muendelezo wa vita vya kiuchumi. Yaani vita vimepamba moto dhidi ya mabeberu na wasaliti wachache waliopo hapa nchini.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mujibu wa bandiko inaonesha hatujafanya hata effort ya kupambana mahakamani. Utashindaje kama hata hujaonesha kuguswa?
kuguswa namna gani kama sio kutoa maoni yangu hapa... kwa mimi binafsi , nashinda mahakamani kila siku na mziki wa huko na technicality za haya mambo nazijua sana Jua liwake winter au kiangazi kije... labda usome tu article hii na utajua kwamba hizi corporate entities huwa tu zinapewa ushindi na walipa kodi kubebeshwa mzigo.. sio tu kwetu Africa bali hata mabeberu wenyewe wanailalamikia hii ISDS... soma hapa article hii usije kusema hukujua: https://corporateeurope.org/sites/default/files/attachments/the_zombie_isds_0.pdf

ukisoma kuanzia ukurasa wa 38 ndio utajua ni kwanini nchi (Karibia zote) huwa zinashindwa kesi maana kama unavyoambiwa kwenye ukurasa wa 36- the devil is in the details... usifikilie kwamba Tanzania ni ya kipee sana kwenye haya mambo ya ISDS .. Vingevenyo ni kujimwambafai tu bila mpango ili kusubiria mabeberu yataje ni kisasi gani yanataka kulipwa na baada ya hapo kuwaomba poo ili tumalizane nao...
 
Kwa mujibu wa bandiko inaonesha hatujafanya hata effort ya kupambana mahakamani. Utashindaje kama hata hujaonesha kuguswa?
na kwa kukusaidia ni kwamba- kesi huwa hazishindiwi mahakamani- kesi zote zinashindiwa kabla ya kwenda huko kwa pilato... mahakamani ni procedures tu kukazia hukumu ya makubaliano ili usipolipa wataifishe mali zako...au kufungwa.. ukweli ni kwamba pambana iwezekanvyo kabla ya kwenda mahakamani vinginevyo itategemea na judge kaamukia upande upi au alikula maharage ya wapi...
 
Hawa washenzi waliopoka dola watatupeleka pabaya tusiache siku yoyote kuwaondoa hata kwa mawe.
Mungu tunusuru maana tumeanza kupigwa toka Kusini, Kaskazini, Mashariki na Magharibi

Ilani ya CCM ina kura 303 . Kwa Hali hii itatekelezwa ?

As you make your bed, so you must lay on it!

Parte after parte

Huwa wanaulizia MIGA wacha waipate fesh.

Lets wait and see

Ofisi ya Attorney general wanaenda front wenyewe? Hawana wanasheria wa nje huko wanaoweza kula sahani moja na Wazungu?

 
''The Ntaka Hill Nickel Project was awaiting Tanzania’s green light for the mining stage up until August 2019 when the license was cancelled.''

Kwa hiyo basi Tanzania hawakutoa green light na hiyo licence ikafutwa. Imekula kwao, sioni kama hapo pana utata miaka 5/6 hawakuweza kufanya kitu ngoja tuone.
 
Safi sana hii........ I really like it. Serikali dharimu lazima iwajibishwe kwa njia tofauti tofauti
 
Safi sana hii........ I really like it. Serikali dharimu lazima iwajibishwe kwa njia tofauti tofauti
Kumbuka lakini uzembe na ujinga wowote wa dereva utatugarimu na tutaumia sisi abiria. Wakati wa kulipa hizo faini hawatatangaza ni wewe utaongezewa kodi utaambiwa mpaka ng'ombe umlipie kodi na ukienda hospital utakosa dawa mana pesa ya kununulia dawa inalipa madeni.
 
Nachingwea UK Ltd (“NUK”)
Nachingwea Nickel Limited (Tanzania)
majina ya makampuni ya Kihuni! Lazima washindwe mapema tu!
 
Kabisa..... Ndivyo inatakiwa iwe labda akili zitatukaa sawasawa..... Sasa hivi ni ubatili mtupu.......
 
Tatizo sio mahakamani bali ni hao kutaka kuendelea kuhodhi hayo maeneo ya uchimbaji bila kuyafanyia kazi. Serikali inaweza kuamua kumalizana nao nje ya mahakama, wakapewa hayo maeneo under the new laws.
 
Ukiwamo wewe uliyelawitiwa ila taifa letu haliwezi kulawitiwa kwa kuwa sio mira zetu,
Hizo mahalama zipo kwa ajiri ya watu mataifa kazi kubwa ni kupambana nao wale wanaotaka kusariti nchi kwa vyovyote vile.
Hao wanasheria hawakuajiliwa kama pambo tu bali ni kwa ajili ya hizo kesi na watazishinda tu kama wamedhamilia kuwa wazalendo na sio wa kwenda kuuza nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…