Kama TBC hawana uwezo wangeingia mikataba na vituo binafsi vya TV kurusha matangazo ya mechi zinazohusu timu ya taifa kwa masharti ya kuonyeshwa pia kupitia TBC 1. Kwa mfano kama mechi inarushwa na Azam TV, basi ionekane kupitia Azam One na TBC 1. Wananchi wana haki ya kuiona timu yao ya taifa.